NECTA yaonya udanganyifu mtihani kidato cha nne...Soma habari kamili na Matukio360...#share
Na Abraham Ntambara
WAKATI kesho wanafunzi wa kidato cha nne wakitarajia kuanza mtihani
wa kumaliza kidato cha nne, Baraza la Mtihani nchini (NECTA) limesema
halitosita kumchukulia hatua mwanafunzi yeyote pamoja wasimizi wa mitihani
hiyo ambao watajihusisha na vitendo vya udanganyifu.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA), Dk. Charles Msonde
Pia, Baraza hilo limewapa onyo wamiliki wa shule kuacha kuwaingilia wasimamizi wa mitihani hiyo
kwakuwa shule zao ni vituo maalum vya kufanyia mtihani.
Onyo hilo limetolewa leo Jijini Dar
es Salaam, Katibu Mtendaji wa (NECTA), Dk. Charles Msonde wakati wa mkutano na
waandishi,amesema Baraza hilo linatoa wito kwa
kwa wasimamizi wa mitihani wote
kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu.
“Tunawaasa wasimamizi wa mitihani
pamoja na wanafunzi kujiepesha na vitendo vya udanganyifu kwani Baraza
litachukua hatua kali kwa
yeyote yule atakayebainika kukiuka taratibu
za uendeshaji wa mitihani ya Taifa” amesema Dk Msonde.
Amesema Baraza hilo linawataka wamiliki wa shule kutambua kuwa shule zao ni vituo maalum vya mitihani na hivyo havitakiwi kuingilia majukumu ya
wasimamizi.
“Baraza halitasita kukifuta
kituo chochote cha Mitihani endapo
litajiridhisha kuwa uwepo wake wa unahatarisha Usalama wa Mitihani ya
Taifa”amesema Dk. Msonde.
Hata hivyo, Dk amesema Baraza hilo
linaamini kuwa walimu wamewaandaa vizuri
wanafunzi hao kwa kipindi cha miaka mine ya elimu ya sekondari hivyo
hakutakuwepo na vitendo vya udanganyifu.
Pamoja na hayo,Amesema katika
mitihani huo Jumla ya watahiniwa 585,938 wamesajiliwa kufanya mtihani wa huo,
ambapo kati yao watahiniwa wa shule ni 323,513 na watahiniwa wa kutegemea ni
62,425.
“Kati ya watahiniwa wa shule
323,513 waliosajiliwa ,wanaume ni 159.103 sawa na asilimia 49.18 na wanawake ni 164,410 sawa na asilimia 50.82,huku
watahiniwa wenye uono hafifu ni 305 ambapo maandishi yao yanakuzwa”amesema Dk. Msonde.
Kuhusu watahiniwa wa kujitegemea
waliosajiliwa ni 62,425 ,wanaume ni 28,574 sawa na asilimia 45.77 na wanawake ni 33,851 sawa na asilimia 54.23
huku watahiniwa 6 wasioona.
Aidha,Baraza hilo linatoa wito kwa
jamii kutoa ushirikiano katika kuhakikisha mitihani hiyo ambayo inaanza kesho
octoba 30 hadi 17 Novemba 2017
inafanyika kwa Amani na Utulivu huku akiwaomba wananchi hao kuheshemu eneo la
mtihani linapofanyika.
No comments:
Post a Comment