Dk Mwaiselage:Tezi dume haipimwi kwa kidole..soma habari kamili na Matukio360..#share
Salha Mohamed
MKURUGENZI Mtendaji
wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk.Julius Mwaiselage amesema saratani ya
tezi dume haipimwi kwa kutumia kidole kama ambavyo taarifa mbalimbali zinavyoeleza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam juu ya matembezi ya hisani ya kuhamasisha Uchunguzi wa saratani ya matiti yatakayofanyika kesho yatakayoanzia katika viwanja vya Taasisi hizo.
Amesema hayo leo jijini
Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matembezi ya
hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa mapema wa saratani ya matiti.
Amesema wananchi
wamekuwa na dhana potofu ya namna ya kupima saratani ya tezi dume na kuwafanya
wanaume kushindwa kujitokea katika upimaji ili kuanza matibabu.
“Watu
hupotosha namna ya upimaji tezi dume, Tanzania imeweka mwongozo wa kupima tezi
dume ambapo wanapima kupitia damu,”amesem.
Amesema
mwanaume hufika kituo cha kutolea huduma za afya na kupima damu kama ambavyo
mgonjwa wa malaria au HIV anavyopimwa.
Amesema
endapo mgonjwa atajulikana na ugonjwa huo daktari atachukua hatua nyingine ya
matibabu zaidi lakini si kwa namna ambavyo wananchi wanavyosema matibabu yake
kwenye mitandao ya kijamii.
Dk.
Mwaiselage amewataka wananchi kuwa na utaratibu wa kupima saratani mara kwa
mara kwani huduma hiyo hutoewa bure kwenye vituo 460 hapa nchini.
Amesema
taasisi hiyo ilihudumia wagonjwa 27,907 ambapo wagonjwa wapya wa saratani 6,338
na wale wa marudio waikuwa 21,569.
“Taasisi
ilifanya uchunguzi wa saratani ya matiti na shingo ya kizazi kwa watu 9,028
ambapo kati yao 1,123 walikutwa na dalili za awali za saatani ya matitina
shingo ya kizazi,”amesema.
Ameongeza
kuwa taasisi hiyo ilifanya uchunguzi wa satarani ya tezi dume kwa wananume 534
ambapo kati yao 27 walikutwa na dalili za awali za saratani.
Amesema
kwenye taasisi hiyo wagonjwa wa saratani
wamekuwa wakiongezeka kila mwaka hadi kufikia mil 14.1 huku mil 8.8
hufariki kila mwaka kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani ya mwaka 2015
ikisababishwa na sababu mbalimbali.
Mkurugenzi wa Kinga
Hospitali ya Agakhani, Dk. Crispin Kahesa amesema saratani haichagui jinsia
ambapo hata waname huwapata ambapo serikali imejenga uwezo wa rasilimali watu
katika kuongeza tiba.
Taasisi hiyo inatarajia
kufanya matembezi ya hisani ya kuhamasisha saratani ya matiti kesho
yatakayoanzia katika taasisi hiyo huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Afya ,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
No comments:
Post a Comment