Dk. Mwaiselage: Tezi dume haipimwi kwa kidole...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Salha Mohamed, Dar es Salaam
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road,
Dk.Julius Mwaiselage amesema saratani ya tezi dume haipimwi kwa kutumia kidole
kama ambavyo mitadao ya kijamii inavyoeleza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam juu ya matembezi ya hisani ya kuhamasisha Uchunguzi wa saratani ya matiti yatakayofanyika kesho yatakayoanzia katika viwanja vya Taasisi hizo.
Ameyabainisha hayo leo jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa
mapema wa saratani ya matiti.
Amesema wananchi wamekuwa na dhana potofu ya namna ya kupima
saratani ya tezi dume na kuwafanya wanaume kushindwa kujitokea katika upimaji
ili kuanza matibabu.
“Watu hupotosha namna ya upimaji tezi dume, Tanzania imeweka
mwongozo wa kupima tezi dume ambapo wanapima kupitia damu,”amesem.
Amesema mwanaume hufika kituo cha kutolea huduma za afya na
kupima damu kama ambavyo mgonjwa wa malaria au HIV anavyopimwa.
Amesema endapo mgonjwa atajulikana na ugonjwa huo daktari
atachukua hatua nyingine ya matibabu zaidi lakini si kwa namna ambavyo wananchi
wanavyosema matibabu yake kwenye mitandao ya kijamii.
Dk. Mwaiselage amewataka wananchi kuwa na utaratibu wa kupima
saratani mara kwa mara kwani huduma hiyo hutoewa bure kwenye vituo 460 hapa nchini.
Amesema taasisi hiyo ilihudumia wagonjwa 27,907 ambapo wagonjwa
wapya wa saratani 6,338 na wale wa marudio waikuwa 21,569.
“Taasisi ilifanya uchunguzi wa saratani ya matiti na shingo ya
kizazi kwa watu 9,028 ambapo kati yao 1,123 walikutwa na dalili za awali za
saatani ya matitina shingo ya kizazi,”amesema.
Ameongeza kuwa taasisi hiyo ilifanya uchunguzi wa satarani ya
tezi dume kwa wananume 534 ambapo kati yao 27 walikutwa na dalili za awali za
saratani.
Amesema kwenye taasisi hiyo wagonjwa wa saratani wamekuwa
wakiongezeka kila mwaka hadi kufikia mil 14.1 huku mil 8.8 hufariki kila mwaka
kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani ya mwaka 2015 ikisababishwa na sababu
mbalimbali.
Mkurugenzi wa Kinga Hospitali ya Agakhani, Dk. Crispin Kahesa
amesema saratani haichagui jinsia ambapo hata waname huwapata ambapo serikali
imejenga uwezo wa rasilimali watu katika kuongeza tiba.
Taasisi hiyo inatarajia kufanya matembezi ya hisani ya
kuhamasisha saratani ya matiti kesho yatakayoanzia katika taasisi hiyo huku
mgeni rasmi akiwa Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto,
Ummy Mwalimu.
No comments:
Post a Comment