Kesi ya Jamali Malinzi 'kizungumkuti'..soma habari kamili na Matukio360..share
Na
mwandishi wetu
WAKILI,
Richard Rweyongeza anayemtetea rais wa
zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Jamal Malinzi na wenzake
umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
kumuita Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai
(DPP) kueleza ni kwanini jalada la kesi
hiyo lipo ofisini kwake kwa muda wa siku 37.
Rais wa zamani wa TFF, Jamali Malinzi wa pili kutokata kulia akiwa Mahakamani
Amewasilisha
ombi hilo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kufuatia Mwendesha
Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard
Swai kudai upelelezi wa kesi hiyo
bado haujakamilika na kuomba ipangiwe tarehe nyingine.
Baada
ya kutolewa kwa maelezo hayo, Wakili Rweyongeza alieleza kuwa upande wa
Mashtaka awali waliomba wiki mbili ili walete taarifa kamili kuhusu jalada
lililopo kwa DPP.
Katika
maelezo ya Swai hatujasikia taarifa ya DPP kuhusu jalada hilo na kwamba wao
walifuatilia.Aliongeza
kudai kuwa wanasita kusema ni matumizi mabaya ya sheria ama ni matumizi mabaya
ya mamlaka ya DPP lakini hakuna lugha nzuri zaidi inabidi waseme hivyo.
Wakili
Rweyongeza aliomba mahakama imuite DPP mahakamani hapo ili afike kueleza kuna
kitu gani ili haki ionekane inatendeka kwa muda anajukumu la kisheria la
kuzingatia haki na kutenda kazi yake kwa kuzingatia haki
Wakili
wa utetezi, Abrahamu Senguji alidai kuwa na yeye alilifuatilia jalada hilo
katika ofisi ya DPP lakini hakupata majibu yaliyomuonesha kuwa DPP yupo makini
hasa katika kesi hiyo.
Hivyo
alidai kuwa kutokana na kutokutenda kazi na kutokutenda Haki DPP mwenyewe aitwe
mahakama ni hapo kueleza ni kwanini jalada hilo limekaa ofisini kwake kwa muda
wa mwezi mmoja na siku saba.
Pia
aliomba mahakama nitumie mamlaka yake kuzuia manyanyaso kwa washtakiwa na
iingilie kati katika suala hilo ili Haki ionekane inatendeka.
Vinginevyo
upande wa Mashtaka wawabadilishie Mashtaka washtakiwa wapate dhamana ili wao
waendelee na upelelezi.
Baada
ys kueleza hayo, Swai alidai kuwa ofisi ya DPP inapokea majalada kutoka nchi
nzima kwa ajili ya kuyatolea maelekezokuhusuana na uchunguzi.
Alidai
kuwa makosa ya kughushi yanahitaji utaalam katika kuyathibitisha na yanachukua
muda mrefu katika uchunguzi.
Aliongeza
katika hili lilipelekwa kwa ajili ya kupitiwa ili atoe kibali liendelee ama
upelelezi zaidi ufanyike ama hakuna ushshidi wa kutosha ifutwe.
Swai
aliongeza kuwa jalada la kesi hii limerejeshwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi
lakini awajapewa taarifa ya maandishi ya kiofisi ndiyo maana hawakulisema hilo
na akaomba ahirisho.
Rweyongeza
alidai kuwa jalada la kesi hiyo tangu Oktoba 5,2017 jalada lipo kwa DPP.
Hakimu
Mashauri atatoa uamuzi wa hoja hizo Novemba 10,2017. Katika kesi hiyo,
washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa
Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga.
Washtakiwa
hao wanakabiliwa na mashtaka 28, yakiwamo ya utakatishaji fedha wa Dola za
Marekani, 375,418.
No comments:
Post a Comment