Habari katika picha: Rais John Magufuli Afanya Mazungumzo na Maseneta wa Baraza la Marekani Ikulu jijini Dar es salaam ..#share

RAIS John Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia Mtukufu Karim Al-Hussaini Aga Khan ambapo ameeleza kuwa  Jumuiya hiyo imedhamiria kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kwa kupanua hospitali ya Aga Khan iliyopo jijini Dar es Salaam na kujenga chuo kikuu kikubwa Afrika Mashariki, Mkoani Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Seneta James Inhofe pamoja na Maseneta wa Baraza la Marekani  walipotembelea na kufanya mazungumzo  Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.

"Upanuzi katika hospitali ya Aga Khan utahusisha kuongeza idadi ya  vitanda kutoka 74 vya sasa hadi kufikia vitanda 172, utaimarisha matibabu ya moyo na kansa  na utaongeza ufundishaji wa madaktari na wataalamu wengine wa afya," amesema Rais Magufuli.

Soma taarifa kamili na Ikulu





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri wa Viwanda Biashara na uwekezaji Charles Mwijage, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamiss Kigwangala, Naibu Waziri wa Mambo ya nje Suzane Kolimba pamoja  Maseneta wa Baraza la Marekani wakiongozwa na Seneta James Inhofe mara baada ya kufanya mazungumzo  Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama kitabu cha Seneta James Inhofe kilichoonyesha picha za maeneo mbalimbali ya Tanzania alipotembelea mwaka mmoja na nusu uliopita, tukio hilo limefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  Seneta James Inhofe pamoja na Maseneta wa Baraza la Marekani walipotembelea na kufanya mazungumzo na mhe, Rais Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia H.H.Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipotembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta  jambo na kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia H.H.Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipotembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na kiongozi waJumuiya ya Ismailia H.H.Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipotembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.


Picha na Ikulu

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search