Jambazi Auawa Kwa Kupigwa Risasi na Wenzake..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share

Na Mwandishi Wetu

MTU mmoja aliyetambulika kwa jina la Robert Massawe (51) mkazi wa jijini Dar es Salaam, anayetuhumiwa kwa makosa ya uporaji na mauaji ameuawa kwa kupigwa riasasi na wautu  wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wenzake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Hamisi Issa, amesema  Kabla ya kuuawa katika majibizano ya risasi baina ya polisi na majambazi , mtuhumiwa alikamatwa akiwa na SMG yenye risasi 24, simu 19 zilizoporwa maeneo mbalimbali na laini za simu 58.

Aidha amesema awali kabla ya kuuawa walikwisha wahi kukamata mtuhumiwa huyo pamoja na mkewe jijini Dar es Salaam ambapo walihojiwa na polisi inadaiwa na alieleza matukio ya ujambazi aliyoshiriki na alikubali kuwaonyesha mahali alipoficha bunduki.

Polisi imesema simu tatu kati ya 19 wamegundua ziliporwa Moshi na moja alikuwa akiitumia mkewe ambaye anashikiliwa Dar es Salaam.

Kamanda Issah alisema aliwaeleza polisi kuhusu mpango wa kufanya tukio la ujambazi katika Kijiji cha Chilio, Kata ya Holili wilayani Rombo jana alfajiri.

Alisema askari walifuatana naye chini ya ulinzi hadi Moshi kwenye dampo lililopo jirani na kiwanda cha ngozi ambako bunduki ilifukiwa ardhini ikiwa na risasi 24.

“Chini ya ulinzi wa askari kanzu, alipowaona wenzake alipiga kelele kuwajulisha polisi walikuwepo eneo hilo,” alisema.

Kamanda Issah alisema kelele ziliwafanya watuhumiwa hao kukimbia huku wakifyatua risasi hovyo na baadhi zilimpiga Massawe mkono wa kushoto, mgongoni na mguuni hivyo kusababisha kifo chake.

Polisi imesema mtuhumiwa alishiriki matukio manane ya uporaji wa fedha na mauaji kwa kutumia silaha na amewahi kufungwa kwa ujambazi lakini aliachiwa baada ya kukata rufaa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search