Baraza la Famasia Mbioni Kutumia Mfumo wa Kielektroniki Kupata Taarifa..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share
BARAZA la Famasia Nchini limesema liko katika mpango wa kuanza kutumia Mfumo Kielektroniki utakaosaidia kupata taarifa za ukaguzi na usimamizi wa huduma kutoka halmashauri zote huku likibainisha kutoa tuzo kwa halmshauri tatu zilizofanya vizuri katika ukaguzi wa dawa na usimamizi huduma.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Msajili wa baraza hilo, Elizabeth Shekalaghe katika Mkutano Mkuu wa 33 wa Mwaka Jumuiya za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Alat) unaoendelea jijini humo.
Amesema baraza hilo linafanya kazi kwa ukaribu na Wakurugenzi pamoja na Wafamasia halmashauri katika kutekeleza majukumu huku akibainisha mfumo huo utasaidia upatikanaji wa taarifa zitakazosaidia na kuwalinda wananchi dawa zisizofaa kimatumizi.
" Tunatambua mchango wa kila halmashauri zote zinafanya kazi vizuri ndio maana tunaendelea kusisitiza ushirikiano katika kuhakikisha taarifa zinapatikana kwa urahisi tunajipanga kutumia mfumo wa kielektroniki," amaesema Shekalaghe.
Amebainisha kuwa katika mwaka wa fedha uliosha mwaka 2015/16 walifanya ukagzi katika halmshauri 37 na kwamba kati hizo halmashauri tatu pekee zilifanya vizuri ikiwemo Halamshauri ya Babati mjinim, Nzega mjini na Mtwara mjini.
Amesisitiza kuwa baraza hilo lilifanya ukaguzi katika maduka madogo na makubwa 1800 ambapo lilibaini asilimia 60 ya maduka hayo kutokidhi vigezo vya kufanya bishara huku asilimia 40 yakikidhi vigezo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Babati Mjini, Faustine Masangu amesema siri ya kupata tuzo hiyo kufanya Vikao vya Kamati ya Chakula na Dawa mara kwa mara ambacho hujadili utekelezaji wa bajeti wa shughuli za ukaguzi na usimamizi wa huduma.
Aidha, amesema katika ukaguzi walikutana na changamoto nyingi ikiwemo uelewa mdogo wa wauza maduka ya dawa, kuyatumia kama zahanati na kukataa kufanyiwa ukaguzi.
Naye Mkurugezi wa Halmashauri ya Nzega Mjini, Philemon Magesa amesema ukaguzi wanaofanya kwa kuzingatia sheria na taratibu ndio uliofanikisha kufanikiwa kudhibiti maduka na zaahanati zisizokuwa na sifa ya kutoa huduma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtwara Mjini, Beatrice Dominick amesema ni jambo la kujivunia halamshauri kuibuka mshindi na kwamba tuzo hiyo imetokana na kufanya kazi kwa kufuata kanuni na sheria za uakguzi.
Na Hussein Ndubikile
No comments:
Post a Comment