NEC Yatangaza Tarehe ya Uchaguzi Mdogo wa Madiwani...Soma Habari Kamili na Matukio360..#share

WAKATI Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema na Mbunge wJospeh Nassari wakiwa wamewasilisha  ushahidi  unaohusu madiwani waliojizulu kwa huku arusha kwa tume ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili hatua zichukuliwe kwa madai madiwani hao wamenunuliwa ili wajuuzulu nafasi zao
Leo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 ikiweni kwenye kata za Arusha ambao utakaofanyika Novemba 26.


Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage amesema uchaguzi unafanyika kutokana na sababu kadhaa, ikiwemo madiwani kufariki dunia, kujiuzulu, kutohudhuria vikao na wengine ushindi wao kutenguliwa na Mahakama.

Miongoni mwa kata hizo ni za madiwani waliojiuzulu mkoani Arusha wakieleza ni kutokana na kumuunga mkono Rais John Magufuli.

Jaji Kaijage katika taarifa iliyotolewa leo Jumatano ametangaza uchaguzi huo mdogo baada ya waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kuitaarifu tume uwepo wa nafasi wazi za madiwani katika kata hizo zilizoko katika halmashauri 36 za mikoa 19 ya Tanzania Bara.

Jaji Kaijage amebainisha kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 kinampa mamlaka waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kutoa taarifa kuhusu kuwepo kwa nafasi wazi za diwani au madiwani katika kata husika.

Amesema baada ya kupokea taarifa hiyo na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 Tume ya Uchaguzi ina wajibu wa kuitisha na kuendesha uchaguzi mdogo katika kata hizo.

"Hivyo, napenda kutumia nafasi hii kutoa taarifa kuwa, tume imepanga kuendesha uchaguzi mdogo katika kata 43 tarehe 26 Novemba, 2017," amesema Jaji Kaijage.

Amesema ratiba ya mchakato wa uchaguzi huo inaanza Oktoba 26 kwa kufanya uteuzi wa wagombea wa udiwani na kampeni zitaanza Oktoba 27 na kumalizika Novemba 25.

Jaji Kaijage amesema vyama vya siasa, wadau wote wa uchaguzi na wananchi wanakaribishwa kwa ajili ya kushiriki kwenye uchaguzi huo.

Ametoa wito kwa vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa (madiwani) za mwaka 2015, maadili ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani ya mwaka 2015 na maelekezo yote yaliyotolewa au yatakayotolewa na tume wakati wote wa uchaguzi mdogo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search