Julitha Kabete kuwakilisha miss word 2017.. soma habari kamili na Matukio360.. #share
Salha Mohamed
KAMATI ya miss Tz imemteua Julitha Kabete kuwakilisha mashindano ya miss word 2017 Sanya nchini China. Kabete alishika nafasi ya tano katika mashindano ya miss Tz mwaka 2016.
Kabete aliyewahi kushika nafasi ya tano katika mashindano ya Miss Tanzania 2016,ameteuliwa kutokana na upeo mzuri wa kujua mambo mbalimbali duniani.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi bendera ya Taifa, Mkurugenzi wa Mashindano hayo Hashim Lundenga amesema hapo awali mashindano yao yalipata misukosuko na kusababisha kutofanya mashindano nchini.
"Mashindano ya urembo yalipata misukosuko lakini msiniulize kwanini nitasema siku nyingine...mashindano ya urembo yana rekodi nzuri tumemchagua Julitha kwasababu anasifa na upeo mzuri wa kujua mambo ya nchi na ushirikiano,"amesema Lundenga.
Amesema mashindano ya Miss Tanzania kwa sasa wamekimbiwa na wadhamini huku akibainisha kuwa tayari kuanza upya.
Ofisa Utamaduni Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Habibu Msammy amesema awali walifungia mashindano hayo lakini wameangalia katiba yao na kuruhusu kushiriki mashindano ya dunia.
"Tunamtakia kila la kheri Julitha katika kuiwakilisha nchi vema na kuonesha mazuri aliyofundishwa kambini, wasichana wengi wajitokeze katika mashindano haya ya urembo,"amesema.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mtendaji, Baraza la Taifa la Sanaa(Basata), Geofrey Mgezeza, Mkurugezni wa Fedha na Utawala, Onesmo Kayanda amesema mashindano ya Miss Tanzania ni la nchi nzima na si la Julitha pekee kwani anawakilisha nchi nzima.
Akitoa shukrani kwa wadhamini wa shindano hilo, Kabete ameishukuru kamati hiyo kumteua na kuahidi kutowaangusha katika mashindano hayo ya dunia.
Julitha aliwahi kushiriki mashindano ya Urembo Afrika , Miss Afrikayaliyofanyika Nigeria mwaka 2016, Miss Dar City Centre, Miss Ilala hatimaye Miss Tanzania 2016.
KAMATI ya miss Tz imemteua Julitha Kabete kuwakilisha mashindano ya miss word 2017 Sanya nchini China. Kabete alishika nafasi ya tano katika mashindano ya miss Tz mwaka 2016.
![]() |
Habib Msammy kutoka Wizara ya Habari, akimkabidhi bendera mwakilishi wa miss word Tanzania 2017, Julitha Kabete |
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi bendera ya Taifa, Mkurugenzi wa Mashindano hayo Hashim Lundenga amesema hapo awali mashindano yao yalipata misukosuko na kusababisha kutofanya mashindano nchini.
"Mashindano ya urembo yalipata misukosuko lakini msiniulize kwanini nitasema siku nyingine...mashindano ya urembo yana rekodi nzuri tumemchagua Julitha kwasababu anasifa na upeo mzuri wa kujua mambo ya nchi na ushirikiano,"amesema Lundenga.
Amesema mashindano ya Miss Tanzania kwa sasa wamekimbiwa na wadhamini huku akibainisha kuwa tayari kuanza upya.
Ofisa Utamaduni Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Habibu Msammy amesema awali walifungia mashindano hayo lakini wameangalia katiba yao na kuruhusu kushiriki mashindano ya dunia.
"Tunamtakia kila la kheri Julitha katika kuiwakilisha nchi vema na kuonesha mazuri aliyofundishwa kambini, wasichana wengi wajitokeze katika mashindano haya ya urembo,"amesema.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mtendaji, Baraza la Taifa la Sanaa(Basata), Geofrey Mgezeza, Mkurugezni wa Fedha na Utawala, Onesmo Kayanda amesema mashindano ya Miss Tanzania ni la nchi nzima na si la Julitha pekee kwani anawakilisha nchi nzima.
Akitoa shukrani kwa wadhamini wa shindano hilo, Kabete ameishukuru kamati hiyo kumteua na kuahidi kutowaangusha katika mashindano hayo ya dunia.
Julitha aliwahi kushiriki mashindano ya Urembo Afrika , Miss Afrikayaliyofanyika Nigeria mwaka 2016, Miss Dar City Centre, Miss Ilala hatimaye Miss Tanzania 2016.
No comments:
Post a Comment