Dk Tulia: Halmashauri wapimeni afya wananchi...soma habari kamili na Matukio360..#share
NAIBU Spika, Dk Tulia
Ackson amezitaka halmashauri zote nchini kuendesha kampeni ya upimaji afya bure
kwa wananchi ili Watanzania wawe na afya njema katika kuelekea uchumi wa
viwanda.
Wananchi waliojitokeza kupima afya bure wakimsikiliza Nibu spika wa Bunge Dk Tulia Ackson (hayupo pichani ) leo wakati akifunga zoezi hilo katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini mbeya..
Ametoa wito huo leo
mkoani Mbeya alipokuwa akifunga kampeni ya upimaji afya bure ambapo
takribani wananchi
13,000 mkoani humo wamejitokeza kupima afya bure iliyozinduliwa Oktoba 14 mwaka huu.
Mganga Mkuu wa Hospitali
ya Mkoa huo, Seif Mhina amesema wamevuka
lengo. Walitarajia kupima wananchi 10,000. Kwa siku wananchi 2,000.
Mhina amesema idadi
hiyo imeonyesha jinsi wananchi walivyohamasika na Oktoba 21,2017 wataendelea na
kampeni hiyo inayoratibiwa na mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. Itafanyia
katika Chuo Cha Uhasibu (TIA).
Kampeni hiyo imefanywa
na wataalam 86 kutoka hospitali ya Mkoa,
Rufaa ya Kanda, Jeshi, na halmashauri saba za mkoani Mbeya .
Pamoja na magonjwa
mengine jumla ya wanaume 195 wamejitokeza kupima ugonjwa wa tezi dume, 26 wamekutwa
na tatizo hilo na kupatiwa matibabu.
Ameitaka jamii kuwa
na mwamko wa kupima afya ili kujikinga na magonjwa nyemelezi ambayo ni
changamoto inayopoteza nguvu kazi kwa
taifa hususan kwa vijana.
No comments:
Post a Comment