Kaimu Mkurugenzi Mkuu TAWA Dkt. James Wakibara akiwa katika mwendelezo wa ziara yake kutembelea mapori ya akiba(Game Reserves) katika Mkoa wa Rukwa, amepata fursa ya kutembelea pori la akiba Uwanda ambalo lipo Wilaya ya Sumbawanga, alikutana na kundi la mifugo Ndani ya Hifadhi waliokamatwa na askari wanyamapori wakiwa wamezungushiwa boma baada ya wamiliki wa ng"ombe hao 319 walikimbia. Uongozi wa pori tayari umefungua kesi mahakamani.
Kaimu Mkurugenzi akizungumza na watumishi aliwapongeza kwa kuchapa kazi hasa kukabiliana na changamoto zinazowakabili zikiwemo kuingiza mifugo hifadhini.
Meneja wa pori Bw. Chuwa amemueleza Kaimu Mkurugenzi mkuu pori hilo changamoto kubwa ni ujangili wa uvuvi haramu, kukata miti kwa ya ajili ya mbao na kuingiza mifugo.
(Imeandaliwa na: Twaha Twaibu(Afisa Habari na Mahusiano - TAWA)
|
Kaimu mkurugenzi mkuu-TAWA .Dkt. James Wakibara akipokea maelezo kuhusu mifugo iliyovamia hifadhi kutoka kwa meneja. wa pori La Uwanda Bw. Mark Chuwa |
|
Kundi la ng'ombe 319 waliokamatwa na askari wanyamapori-TAWA |
|
Dkt. Wakibara (wa 5 kutoka kushoto) akiwa na watumishi wa pori la akiba Uwanda |
|
Dkt Wakibara anaongea na watumishi wa Uwanda |
|
Pichani juu ☝️na chini 👇 Dkt. Wakibara akipata maelezo ya mpaka kwenye ramani Kati ya vijiji Jirani na pori la Uwanda kutoka kwa Meneja wa Uwanda Bw. Chuwa |
Pichani Juu ☝️Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za ulinzi wanyamapori Bw. Mabula Misungwi (kulia)
akimsikiliza kwa makini Dkt. Wakibara kuhusu udhibiti wa mpaka
No comments:
Post a Comment