Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita Atoa Rai Wajumbe wa ALAT Kujadili Maslahi ya Madiwani Nchini..Soma Habari Kamili na Matukio360...#share
MEYA wa Jijini la Dar es Salaam Isaya Mwita ametoa rai kwa Wajumbe
wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ALAT) kujadili kwa kina changamoto za
kimaslahi zinazowakabili madiwani ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao
katika mazingira mazuri.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam akizungmza mbele ya wajumbe wa ALAT wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa 33 jijini hapa.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati wa
ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Siku tatu wa ALAT, amesema hii ni moja changamoto
kubwa ambayo wamekuwa wakabiliana nayo ni kwenye suala la maslahi hususania
katika posho zao.
Amebainisha kuwa madiwani wamekuwa wakikabiliwa na wakati
mgumu katika kuhakikisha wanasimamia shughuli za kila siku kutokana na kulipwa posho ndogo ya sh. 350000 ukilinganisha na gharama ya maisha ya sasa kuwa juu.
“Diwani analipwa sh.350,000, diwani anakaa Dar es Salaam ama
anakaa Mwanza au katikati ya mji, kuzunguka lazima atumie gari, mafuta na vitu
vingi, kwa hiyo ifike sehemu nadhani katika kikao hiki tunapokuwa tukifanya
uamuzi ni vyema serikali ikaangalia namna ya kupandisha hizi posho za madiwani
ambazo kimsingi hazikidhi kulingana na maisha ya sasa,” amesema Mwita.
Ameongeza “Niwaombe ndugu zagu wajumbe wa ALAT naelewa katika
kipindi hiki tukiwa hapa, tutapata muda mwingi wa kujadili mambo yetu ya ALAT,
tena bahati nzuri tutakuwa na mgeni ambaye tumekuwa tukimkosa kwa muda mrefu,”.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na waandishi wa habari baada ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa ALAT leo Jijini hapa.
Aidha Mwita akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi
wa mkutano huo amesema pamoja na kujadili maslahi ya madiwani, watapata muda wa
kuzungumzia changamoto zinazokabili halimashauri ili kuhakikisha zianakuwa na
Afya njema.
Amebainisha kuwa changamoto inayokabili halmashauri zote
nchini ni kuondolewa kwa mapato ambayo zilikuwa zikikusanya kutokana na
makusanyo hayo kuchukuliwa naserikali kuu.
“Mtakumbuka kwamba vyanzo vingi vilirudishwa serikali kama
propet tax, Mabango, kwa hiyo kupitia kikao hiki naamini kwamba kwasababu
anakuja mheshimiwa Rais atapewa salamu hizi na atapewa ujumbe huu kwa afya ya
hizi halmashjhauri,” amesema Mwita.
Ameeleza kuwa kupitia kikao hicho Watatoka na maazimio ambayo
wanaamini Rais John Magufuli na Serikali yake watayachukua na kuyafanyia kazi
kwa ajili ya afya za halmashauri zote nchini.
Na Abraham Ntambara
No comments:
Post a Comment