Kamati Maalum Yalaani Kukatwa Mkono Mzee Msigili..Soma Habari Kamili na Matuki0360..#share

KAMATI Maalum ya Kuhamasisha Jamii kuwajali na kuwathamini watu wenye Ualbinp kwa njia ya Mpira wa Samatta imelaani vikali tukio la kukatwa mkono Mzee Nassoro Msingili(75) lililotokea Oktoba 3 mwaka huu mkoani Morogoro.
Image result for Mwenyekiti wa kamati maalumu ya uhamasishaji  Michael Lugendo

Aidha, imesema kitendo hicho ni cha kinyama na hakikubaliki hata kidogo na kuiomba Serikakali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk John Magufuli kuchukua hatua madhubuti kukomesha vitendo vya kuwadharau watu hao kwani wanastahili kuishi kama binadamu wengine.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa taasisi ya Albino Enterpses of Dar es Salaam, Michael Lugendo wakati akitoa ufafanuzi wa tukio hilo.

Amesema vitendo hivyo vimeshindwa kufikia ukomo kutokana na jamii kuendelea kuendekeza dhana potofu zinazochangia mauaji wa watu wenye ualbino huku akiwaomba watu wenye mapenzi mema na jamii ya watu hao kuunga mkono kampeni ya kuwajali na kuwathamini maalbino ili waweze kusambaza elmu ya kutokomeza imani za kishirikina zinazosababisha maovu hayo.

A mebainisha kuwa kamati hiyo inampongeza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei  ambaye  pia ni mjumbe wa kamati kwa kuchukua hatua za haraka na kuwakamata watuhumiwa wa mauaji hayo hadi sasa.

Amewashukuru wadau mbalimbali zikiwemo kampuni na vyombo vya habari kwa ushirikiano mkubwa wanaoendelea kuutoa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search