Sitta Awataka Wenyeviti na Watendaji wa Serikali za Mitaa Kuwa Waadilifu..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share

Na Mwandishi Wetu
MEYA wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta amewakata wenyeviti na watendaji wa mitaa kuwa waadilifu na wabunifu katika sehemu zao za kazi ili kupunguza kero za wanachi.
Meya wa Kinondoni Benjamini Sitta akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya watendaji na wenyeviti wa Serikali za Mitaa jijini Dar es Salaam Leo.
Sitta amesema hayo leo wakati akifungua semina ya watendaji na wenyeviti hao ambayo imeratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam yenye lengo la kuwajengea uwezo katika utekelezaji wa majukumu yao katika kuwatumikia wananchi, na amewataka kubadililika kuendana na wakati uliopo katika utoaji wa huduma.
Amewataka kutokuwa na vinyongo wakati mambo yanapokuwa yameamriwa bali kutoa maoni yao kwa Manispaa ili kuboresha utendaji kazi na kuleta maendeleo katika manispaa hiyo.
Aidha, amesema kuwa utaratibu wa kutuma barua kwa mkono umepitwa na wakati , na kwamba utaratibu wa kutumia mfumo wa kisasa unaandaliwa ili kurahisisha utoaji huduma kwa wanachi.
Ameongeza kuwa Manispaa hiyo inakabiliwa na migogoro mingi ya ardhi kuliko sehemu yoyote Tanzania huku akibainisha kuwa baadhi yao wamechangia tatizo hilo, na kuwataka kuainisha maeneo yote yasiyoendelezwa kwa muda mrefu na maeneo ambayo hayajapimwa pamoja na maeneo ya uwekezaji.
Nao baadhi ya wenyeviti wa na watendaji wa mitaa waliohudhuria semina hiyo wamesema kumekuwa na changamoto kubwa ya njia nabarabara katika maeneo yasiyo pimwa na yamekuwa yakisababisha shida kubwa na ufinyu wa njia kubanana kwa mitaa na kusababisha maeneo mengi kuwa machafu kwa sababu ya baadhi ya wananchi kutochangia gharama za usafi wa uzoaji taka.
“kumekuwa pia na wafanyabiashara ndogo hawa wamachinga wanakaidi maelekezo wanapanga bidhaa zao hadi barabarani hapa maeneo ya kwa Ndevu Tegeta kwa kisingizio kuwa Rais amewaruhusu kufanya biashara na wengine wamejenga vibanda katika mtaro wa TANRODS, kwa kweli hili na ni kero na halikubaliki kabisa lazima waheshimu miundombinu na tutawahamisha ‘’ . Amesema Luteni Kanali Mstaafu wa Mtaa wa Tegeta Ahaba Lwiva .
No comments:
Post a Comment