Kesi ya Mwenyekiti CCM Yapigwa na Wenzake Yapigwa Kalenda'..Soma Habari Kmili matukio360..#shar
KESI inayomkabili Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge
wa Geita Joseph Msukuma na madiwani nane
imesogezwa mbele baada ya upande wa mashitaka kudai upelelezi haujakamilika.
Mbunge wa Jimbo la Geita,na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoani Geita ,Joseph Kasheku(Msukuma) akiteta jambo nje ya mahakama baada ya kesi kuhailishwa
Kesihiyo ambayo ilikuwa isikilizwe
leo imepangwa kutajwa tarehe 10 mwezi wa 11 mwaka huu ambapo washitakiwa wote
wapo nje kwa dhamana.
Kwa upande wake wakili anayewatetea
washitakiwa Bw Deo Mgengeli ameelezea hatua ambayo imeendelea siku ya leo
mahakamani hapo kuwa shauri limekuja na kwamba limetajwa na hadi sasa hakuna
mshitakiwa ambaye ameongezeka hivyo mahakama imeamua tarehe Kumi mwezi wa 11
wawasili mahakamani kusikiliza tena kesi hiyo.
Aidha wakili Mgengeli amezungumzia
suala la madiwani wengine waliokamatwa na jeshi la polisi na kutofikishwa
mahakamani amesema kuwa kukamatwa kwa madiwani hao ni jambo
la kawaida kwani ni swala la upepelezi kwa makosa ya jinai na kwamba
alhamisi wanatakiwa kwenda tena polisi ili kujua ni kipi ambacho kinaendelea ila
hadi sasa awana kosa lolote.
Awali washitakiwa hao kwa pamoja
walifikishwa
katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita Septemba 19 mwaka huu.
katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita Septemba 19 mwaka huu.
Washitakiwa wanakabiliwa mashitaka
ya kufanya mkutano bila kibali, kuziba barabara na uharibifu wa bomba la maji linaloelekea kwenye mgodi wa dhahabu wa GGM.
Baadhi ya wananchi ambao walijitokeza kusikiliza kesi hiyowakiwa nje ya mahakama. |
No comments:
Post a Comment