Katibu mkuu mpya Madini atoa tahadhari kwa watendaji..Soma habari kamili na Matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu mpya wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila amewataka watumishi wa wizara hiyo kuwajibika katika nafasi zao ili wananchi wanufaike na matunda ya kazi  kama inavyopaswa.
Katibu Mkuu wa Madini, Profesa Simon Msanjila akisalimiana na wafanyakazi wa wizara hiyo leo mkoani Dodoma

Profesa Msanjila ameyasema hayo leo Oktoba 30, 2017 baada ya kuwasili rasmi Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma na kupata fursa ya kuzungumza na wafanyakazi.

Amefafanua kuwa, uwajibikaji hupimwa kwa matokeo. "Tutakuuliza umefanya nini katika nafasi yako ili tuweze kupima utendaji wako."

Aidha, Profesa Msanjila amesisitiza ushirikiano baina ya viongozi na wafanyakazi wote ili kupata matokeo chanya, hivyo kuleta manufaa katika sekta ya madini.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa Wizara ya Madini, Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, ameahidi ushirikiano kutoka kwa wafanyakazi na uwajibikaji katika nafasi zao kama alivyoasa Katibu Mkuu.

Katibu Mkuu Msanjila, amepokelewa na watumishi wa Wizara husika, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Lusias Mwenda.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search