MAGUFULI: Mimi ni kibarua, Meli mpya kutengenezwa...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Mwandishi wetu
RAIS Dk John Magufuli
amesema yeye ni kibarua wa Watanzania na kwamba pamoja na changamoto zote
atawatumika kwa moyo wa uadilifu na uaminifu.
Rais wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli
Pia amesema Serikali
itatengeneza Meli mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 1200 na kupanua uwanja wa
ndege jijini Mwanza.
Ametoa kauli hiyo Leo
jijini Mwanza alipokuwa akifungua rasmi matumizi ya daraja jipya la waenda kwa
miguu la Furahisha. Linauwezo wa kupitisha watu 60 kwa wakati mmoja
“Mimi ni kibarua
wenu, nitakutumikieni kwa moyo mmoja. Naamini kila kitu kipya ni miujiza na
haya ninayofanya na kuahidi ni kama miujiza lakini namuomba Mungu iwe kweli, ” amesema
rais Magufuli
Amesema daraja hilo
lililochorwa na waadisi na kujengwa na wakandarasi wazalendo halipo mahala popote nchini.
‘Jamani
haya ndio maendeleo pamoja na mambo mengine limejengwa na wazalendo na halipo
mahala popote nchini. Linajiwasha taa lenyewe,’ amesema
Rais
amesema mkakati wa serikali ni kuufanya mkoa wa Mwanza kuwa kiunganishi katika
biashara na kwamba itatengeza meli mpya.
Amesema
kampuni moja kutoka Korea Kusini imeshinda tenda ya utengenezaji wa meli hiyo
itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria zaidi 1200, tani za kutosha za mizigo na
magari.
‘Tayari
hawa watu wa Korea Kusini wameshafika
hapa Mwanza tangu jana jioni na leo wataanza kukagua mahala pazuri pa kujengea
hiyo meli, wakikamilisha hayo tutasaini mkataba na mwisho wa mwezi wa kwanza,
2018 ujenzi utaanza,’ amesema rais
Mbali
na meli hiyo, rais Magufuli amesema serikali itazifanyia ukarabati meli ya Mv
Victoria na Liemba ya mkoani Kigoma ziweze kuwa katika ubora.
Amesema
fedha zote zinatolewa na serikali na kwamba upanuzi wa uwanja wa ndege wa
Mwanza utaanza mara tu baada ya mazungumzo kati ya serikali, wahisani na
wafadhili kukamilika. Amesema
lengo ni uwanja wa ndege wa Mwanza kuwa wa kimataifa.
Rais
ameongeza kuwa ujenzi wa barabara mpya inayowekwa lami ya kutoka Kisesa kwenda
Usegera umekamilika kwa asilimia 80 lengo ni kupanua uchumi wa Mwanza.
Amesema
upembuzi yakinifu unafanyika wa ujenzi wa barabara wa kilomita tatu za lami kutoka
Busisi hadi Kigongo. ‘Pia tunazifanyia uboreshaji na upanuzi
hospitali za Mwanza ikiwamo ya seketule,’ amesema
Pamoja na mambo mengine
amesimamisha bomoabomoa za nyumba katika
baadhi ya maeneo jijini humo.
No comments:
Post a Comment