Kenya: Odinga Ajiondoa Kwenye Kinyang'anyiro cha Urais..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share

MGOMBE Urais wa Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya National Super Alliance (NASA) Raila Odinga ametangaza kujiondoa kugombea urais wa Kenya, kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu.
Akitangaza hatua hio leo, Odinga amesema Miongoni mwa sababu kubwa zilizomsumkuma kuchukua uamuzi huo ni pamoja na umoja huo wa NASA kuhisi Tume ya Uchaguzi nchini humo IEBC kuwa haina nia ya kuhakikisha yale makosa yaliyosababishwa kufutiliwa mbali matokeo ya urais Augost 8 kuwa hayatajirudia tena.

Pia wameona wapianzani wa Jubilee wanataka kufanyia Katiba mapinduzi na kurudisha udikteta, wanaona kuwa Jubilee wanataka tu kuwe na uchaguzi ila wao wanataka uchaguzi bora.

Aidha wameongeza kuwa Tume hiyo haijafuata masharti waliyotoa ambayo yangeakikisha kuwepo kwa uchaguzi bora na wa haki.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search