Shindano la StarTimes Kusaka vipaji vya Sauti, Usaili Mwanza wafunika..Soma Habari Kamili na Matukio360..#share
HATUA ya usaili katika shindano la kusaka vipaji vya sauti linalodhaminiwa na
kampuni ya Star Media Tanzania Ltd ambao ni wamiliki wa Chapa ya StarTimes, ulifanyika
mwishoni mwa wiki iliyopita Oktoba, 7 mwaka huu jijini Mwanza, ambapo mchuano ulikuwa mkali.
Katika usaili huo uliofanyika jijini humo mamia, wake kwa
waume na walemavu pia walifika kuonesha umahiri wao katika kuingiza Sauti.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na
Kitengo cha Mshusiano cha kampuni hiyo ni kwamba, usaili ulianza majira ya Saa
tatu Asubuhi huku majaji wakiwa na wakati mgumu kuchagua wachache ambao
wataingia hatua ya fainali baadaye mwisho wa Mwezi huu jijini Dar es Salaam.
Kutokana na ushindani mkubwa baina ya washiriki, majaji
walipendekeza majina kumi na moja badala ya mnajina kumi kuingia raundi ya
mwisho jijini Mwanza, washiriki wawili walipata Alama sawa hivyo wote wakaingia
hatua iliyofuata. Licha ya ushindani huo mwisho wa Siku ni majina matano tu
ndiyo yalibahatika kuingia hatua ya fainali.
Miongoni mwa washiriki hao ni msanii wa Muziki wa kizazi
kipya “Pipi”. Pipi alionyesha uwezo mkubwa wa kuingiza sauti na hivyo kupata
nafasi ya kuingia fainali ya Shindano hilo jijini Dar es Salaam mwisho wa mwezi
huu.
Wikiendi hii ni zamu ya Dar es Salaam, usaili utafanyika
katika fukwe za bahari, Coco Beach Siu ya jumamosi tarehe 14 mwezi wa 10.
“Washiriki ambao wamekwishajiandikisha hadi sasa ni zaidi ya 700 na tunategemea
wengine zaidi kwa muda uliobaki,” alisema Bi. Li Kun, ambaye ni Mkurugenzi wa
Masoko, Star Media (T) Ltd.
Huu ni msimu wa pili wa Shindano hilo la Kusaka vipaji vya
Sauti katika tamthiliya na filamu za kigeni, Msimu wa kwanza ulifanyika mwaka
jana ambapo idadi ya washindi kumi walipatikana na tayari saba kati yao wapo
nchini China wakifanya kazi. Msanii wa maigizo, Nyamayao ni miongoni mwa
washindi wa mwaka jana na tayari ameshatua nchini kwa ajili ya kutioa hamasa
kwa watanzania kushiriki katika shindano hilo.
“Ni nafasi ya kipekee ya kutumia kipaji chako, kufanya kazi
na kukitangaza Kisawahili kimataifa. Kwa muda mabao tumekuwa China,
tumepata nafasi ya kushiriki midahalo na
makongamano mbalimbali ambayo yametuwezesha kuwasilisha Utamaduni wa kitanzania
kwa Ulimwengu” alisema Nyamayao.
Star Media (T) Ltd kupitia nembo ya StarTimes ndio wamiliki
na wadhamini wa shindano hili la vipaji vya Kuingiza Sauti.
No comments:
Post a Comment