Waziri Ummy kuchangia damu wagonjwa wa saratani..soma habari kamili na matukio360..#share
Na
Salha Mohamed
WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ataongoza matembezi
ya hisani kuhamasisha na kutoa elimu ya
saratani ya matiti na kuchangia damu.
Waziri Ummy Mwalimu
Matembezi
hayo yatafanyika Oktoba 28, 2017 kuanzia Taasisi ya Ocean Road hadi Stesheni na
wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi
kuchangia damu kwa wagonjwa wenye saratani.
Akizungumza
na Matukio360, Meneja Uchunguzi wa satarani na Elimu kwa Umma taasisi ya Ocean
Road, Dk Maguha Stephano amesema asilimia 12 ya wagonjwa wapya wanaofikishwa
katika taasisi hiyo wanaumwa saratani ya matiti.
"Mwaka
2006 hadi 2015 inakadiriwa wagonjwa 6000 walipimw kati yao wagonjwa 900
wanasaratani ya matiti, "amesema.
Amesema taasisi hiyo kwa sasa imepokea wasichana
wenye miaka 25 wakiwa na saratani ya matiti hali inayochangiwa na vihatarishi
kadhaa.
Amesema
sababu za kimaumbile ni moja ya vihatarishi vya saratani, wanawake ndiyo waathirika zaidi na kwamba
wanaume ni hatari zaidi.
Dk
Stephano amesema wananchi wajitokeze kwa wingi
katika matembezi hayo na kuchangia damu wagonjwa wa saratani kwa kuwa matibabu
yao huitaji damu nyingi.
"Kutakuwa
na uchunguzi wa saratani ya matiti, utoaji damu kwa wagonjwa wa saratani kwani
huwa na upungufu wa damu hasa wale wenye vidonda vinavuja damu, "amesema.
Amesema
wapo wagonjwa wenye saratani ya damu hivyo huwa na uhitaji wa damu mara kwa
mara.
No comments:
Post a Comment