Kesi ya Kitilya wenzake mambo magumu..soma habari kamili na Matukio360..#share
Na mwandishi wetu
Mwenyekiti
wa Kampuni inayoshughulikia uwekezaji wa
mitaji na dhamana (Egma), Harry Msamire Kitilya na waliokuwa maofisa wa benki
ya Stanbic, Shose Mori Sinare na Sioi Graham Solomon wanaendelea kusota
rumande kutokana na upelelezi wa kesi inayowakabili bado haujakamilika.
Harry Msamire Kitilya katikati na waliokuwa maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Mori Sinare kulia na Sioi Graham Solomon kushoto
Leo
wakili wa Serikali, Esterzia Wilson amedai
mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi
kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Pia
amedai kuwa bado wanasubiri awamu ya pili ya upelelezi kutoka nchini Uingereza.
Hivyo akaomba kesi hiyo ipangiwe tarehe
nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Hakimu
Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi
Novemba 3,2017 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa
umekamilika ama la.
Kesi
hiyo inasikilizwa na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha.
Awamu
ya kwanza ya vielelezo hivyo kutoka
nchini Uingereza vimekwisha pokelewa na
kwamba bado wanasubiri awamu ya pili.
Washtakiwa
hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu
na kutakatisha fedha.
Wanadaiwa
kutenda makosa hayo kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa
mkopo wa dola za Marekani 550 milioni
kwa serikali ya Tanzania kutoka
Benki ya Standard Uingereza.
Wanadaiwa
kuwa Machi 2013 jijini Dar es Salaam
walijipatia Dola za Marekani 6 milioni, wakionyesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni
malipo ya ada ya uwezeshaji upatikanaji wa mkopo na zililipwa kupitia Kampuni ya Egma T Ltd.
Washtakiwa hao wanadaiwa
kutakatisha fedha kwa kuhamisha, kuchukua na kuweka kiasi cha Dola za
Marekani 6 milioni katika akaunti tofauti tofauti za benki.
No comments:
Post a Comment