Kesi ya Lulu dhidi ya Kanumba,mke wa Dk Slaa atafutwa...soma habari kamili na Matukio360...#share

Na mwandishi wetu
KESI inayomkabili msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael 'Lulu' imeendelea leo huku  Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ameamuru askari Polisi aliyechukua maelezo ya mke wa Dk Wilbroad  Slaa, Josephine Mushumbus ambaye ni shahidi wa pili wa upande wa utetezi katika kesi ya mauaji bila kukusudia, kufika mahakamani hapo kesho.



 Msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu'
Jaji wa mahakama hiyo Sam Rumanyika ameamuru  hivyo leo wakati  wa kusikiliza ushahidi wa upande wa utetezi.

Uamuzi huo umefikiwa  baada  ya Wakili wa utetezi, Peter Kibatala kudai  jitihada za kumpata mke huyo wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema kushindikana kwa kuwa yupo nje ya nchi na kwamba wanaomba  kuyasoma na kuyatoa maelezo hayo ili mahakama iyatumie kama kielelezo cha upande wa utetezi.

Kutokana na hali hiyo, Wakili wa Serikali, Faraja George alipinga maelezo ya Wakili Kibatala kwamba anazifahamu sheria hivyo alitegemea kwa kuwa aliyetoa maelezo polisi hapatikani, basi angeletwa  aliyeandika maelezo hayo ili aweze kutoa taarifa hiyo.

Amedai  Kibatala hana mamlaka ya kutoa taarifa hiyo wala kusoma kwani hawezi kuvaa viatu vya watu wote badala yake atabaki kumuwakilisha mteja wake hivyo afuate taratibu zilizowekwa.

Akitoa uamuzi huo, Jaji Rumanyika amesema swali la msingi ni nani atakayeitoa taarifa hiyo mahakamani kati ya wakili na aliyeandika maelezo.

"Kupatikana kwa shahidi imekuwa ngumu lakini anayepaswa kutoa maelezo hayo ni yule ambaye imeshindikana kufika mahakamani hapo na mwengine anayetakiwa kutoa maelezo hayo ni askari Polisi namba E 103 Nyangea. Hivyo, askari huyu anatakiwa kuja kesho kutoa maelezo na hati ya wito apatiwe," amesema Jaji Rumanyika.


Katika kesi ya msingi namba 125 ya mwaka 2012, inadaiwa kuwa Aprili 7,  2012 Sinza Vatican jijini Dar es Salaam, Lulu alimuua Msanii wa filamu, Steven Kanumba bila kukusudia.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search