Afisa TRA mbaroni amiliki gari 19...soma habari kamili na Matukio360...#share

Na mwandishi wetu
AFISA Msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kisutu akikabiliwa na mashtaka mawili ikiwamo la kukutwa akimiliki magari 19,  mali isiyolingana na kipato chake halali.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jennifer ameshtakiwa chini ya kifungu cha 27, (1) (a) na (b) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11ya mwaka 2007.

Akisoma hati ya mashtaka Leo Wakili wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amedai kuwa mshtakiwa huyo  kati ya Machi 21,2016 na Juni 30,2016  jijini Dar es Salaam  akiwa  mwajiriwa wa TRA kama Afisa Forodha Msaidizi alikutwa akimili magari 19.

Magari hayo ni, Toyota Mark X, Toyota Dyna Truck, Toyota Vizt, Suzuki Carry, Toyota Ipsum, Toyota Wish, Toyota Mark II, Toyota Wish  na Toyota RAV4

Mengine ni Toyota Noah,Toyota Regiusage, Toyota Estimated, Toyota Alex, Toyota Crown,  Toyota Hiace, Toyota Estima, Toyota Passo na Suzuki Carry yote yakiwa na thamani ya Sh 197,601,207 mali ambayo hailingani na kipato chake halali.

Wakili huyo wa Serikali Mkuu,  Vitalis amedai  mshtakiwa huyo kati ya Machi  21 ,2012 na  Machi 30,2016 Dares Salaam akiwa mwajiriwa wa TRA kama Afisa Forodha Msaidizi alikutwa akiishi maisha ya kifahari  yenye thamani ya Sh 333,255,556.24 fedha ambayo hailingani na Kipato chake halali.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo mshtakiwa huyo alikana na upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Wakili wa mshtakiwa huyo, Elisaria Mosha aliiomba Mahakama kumpatia dhamana mteja wake wa masharti nafuu.

Hakimu Shaidi, alimtaka mshtakiwa huyo kuwa na mdhamini mmoja anayeaminika ambaye alisaini bondi ya milioni 20. Mshtakiwa huyo alikamilisha masharti hayo ya dhamana na kuachiwa huru. Kesi imeahirishwa hadi Novemba 7,2017 kwa,ajili ya mshtakiwa huyo kusomewa maelezo ya awali

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search