Lema, Heche watoa neno uteuzi DC Mnyeti kuwa mkuu wa mkoa...Soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Mwandishi Wetu
WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
Godbless Lema wa Arusha Mjini na John Heche wa Tarime vijijini wameshangazwa na
hatua ya Rais John Magufuli kumteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Arumeru Alexander
Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema
Kwa nyakati tofauti wabunge hao kupitia kurasa zao za
mitandao ya kijamii wameonesha kukosoa hatua hiyo kutokana na kwamba Mnyeti
bado anakabiliwa na tuhuma ya kununua kwa kuwahonga madiwani wa Chadema Mkoani
Arusha na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM) suala ambalo bado lipo chini ya uchunguzi
wa Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Takukuru)
Kupitia ukurasa wa twitter Heche amesema “Unasema unapiga
vita rushwa na ufisadi mtu anatuhumiwa kufanya vitendo vya rushwa bado
anachunguzwa unampromote! Unatuma mesegi gani Takukuru?,”
“Ni wazi sasa kwamba nchi hii ni mali ya mtu mmoja akimtaka
mtu hata kama ni mchafu kiasi gani sawa na kama hakutaki ukiwa msafi
utachafuliwa,” ameongeza.
Kwa upande wake Lema kupitia ukurasa wake wa twitter amesema Takukuru
walipewa ushahidi wakasema ni ushahidi mgumu lakini DC Mnyeti mwenyewe alitoa
ushahidi kwa kusema kuwa amenunua madiwani wengine Zaidi ya 20.
Ameeleza kuwa mtua hawezi kuonyesha ujasiri kama huo kwenye
suala nyeti kama hilo na bado akabaki kazini.
“Kuna watu katika taifa hili hata wakiua hadharani hawaguswi
ila kuna wengine wanaobambikizwa makosa,” amesema Lema.
Aidha ameongeza kuwa Mnyeti anatuhumiwa na Mbunge wa Arumeru
Mashariki Joshua Nassari (Chadema) kuwa ameshiriki kununua madiwani 10 wa
Chadema kwa rushwa na kuwasilisha ushahidi Takukuru.
No comments:
Post a Comment