Mbunge 'Ssebo' kizimbani kwa kukojoa hadharani,.. soma habari kamili na Matukio360...#share

Mahakama moja nchini Uganda imempiga faini ya Shilingi 40,000 za Uganda mbunge mmoja nchini humo kwa makosa ya kukojoa hadharani.
kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya Mbunge Ibrahim Abiriga wa manispaa ya Arua siku ya Jumanne aliwasili mbele ya mahakama ya mji wa Kampala na kushtakiwa kwa kukojoa katika ukuta wa jumba la wizara ya fedha.


Alikiri kufanya makosa hayo na akaachiliwa baada ya kulipa faini.
Kwa mujibu wa gazeti hilo Kiongozi wa mashtaka aliambia mahakama kwamba mbunge huyo alifanya makosa hayo mwezi Septemba 25 mwaka huu katika barabara ya Kyaggwe mjini Kampala.
Upande wa mashtaka ulisema kuwa vitendo vya mbunge huyo vilikuwa kinyume na sheria za baraza la manispaa ya Kampala za 2016.
Kukiri kwake kunajiri baada picha kadhaa za yeye akikojoakando kando ya barabara kusambaa katika mitandao ya kijamii.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search