Lema, Nassari Watoa Ushahidi wa Rushwa Inayowakabili Madiwani Waliohamia CCM Kumuunga Mkono JPM... Soma Habari Kamili na Matukio360..#share .

MBUNGE wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari ameweka hadharani ushahidi wa rushwa na waliopewa madiwani ambao wamejiuzulu Chadema.        

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili, Nassari ambaye ameambatana na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless  Lema walitoa  ushahidi huo na kueleza wataukabidhi Takukuru na katika taasisi nyingine.

Katika ushahidi huo viongozi kadhaa wamerekodiwa wakiwashawishi madiwani kuhama na baadhi waliahidiwa wangelipwa posho za vikao vyao vilivyobaki hadi 2020 na kukamilishwa  miradi  yao.

Miongoni mwa makubaliano hayo ni kuwa wapewe fedha na kupata ajira na kukamilishwa miradi yote ya maendeleo waliyoahidi.

Wakati Nassari akifanya hivyo tayari baadhi ya madiwani waliojiuzulu walisema kuwa hawakushawishiwa na mtu yeyote wala kupewa rushwa bali wamehama kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search