Mbunge Joseph Haule..Professor Jay Chadema..Asimulia Kwa Uchungu Alivyobomolewa Jumba Lake Mbezi Bila Kuokoa Chochote..Soma Taarifa Kamili na Matukio360..#share
Anaandika Mbunge wa Mikumi Joseph Haule (Professor Jay).
________________________________________
________________________________________
Mimi ni mmoja wa wahanga wa hili zoezi la kubomolewa nyumba zetu huku Mbezi Kimara Tarehe 29/9/ 2017.
Jana (Juzi) nikiwa katika majukumu jimboni Mikumi Majira ya saa kumi
mbili hivi jioni, nilitaarifiwa kwamba, watu wa Tanroads wakiwa wameambatana na
grader mbili na magari mawili ya polisi (defenders) yenye askari waliokuwa na
silaha mbalimbali za moto walikuwa wanabomoa nyumba yangu.(sijawahi kuumia
kiasi hiki 😭).
Nimesikitishwa sana jinsi Tanroads wanavyoweza kujichukulia
maamuzi bila ya kujali mhimili muhimu wa Mahakama wametoa maagizo gani. Na
taratibu zilizotumiwa kubomoa nyumba yangu bila ya mimi na Tanesco kupewa
taarifa saa kumi na mbili jioni (haukuwa muda wa kazi).
Poa kubomoa nyumba huku
Umeme ukiwa unawaka ni kitendo ambacho kwanza kina hatarisha maisha ya
wabomoaji wenyewe, maisha ya familia yangu pamoja na majirani zangu,
LIMENISIKITISHA zaidi.
Nasema hivi kwasababu Tanesco wamenipigia simu baada ya masaa
24 au zaidi baada ya zoezi la kubomoa nyumba kufanyika kunitaarifu kuja kukata
Umeme kabla ya ubomoaji huo, pindi nilipo waambia kwamba mbona nyumba
IMESHABOMOLEWA kabisa na sijaweza kuokoa kitu chochote na hata hiyo meter yenu
mnayoiulizia mkaitafute kwenye kile kifusi cha nyumba yangu kilichokusanywa kwa
pamoja na watu wa Tanroads. Tanesco walishangazwa sana kuvunjwa nyumba yangu
kwa taratibu hizo.
Lakini naamini kila kitu kinatokea kwa sababu maalum.
Nimejifunza kumtegemea Na kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Na hili ni moja ya
mitihani ya hapa duniani. Nimepokea na kumsikiliza Mungu ana mipango gani juu
yetu katika familia yangu mbeleni. Tumelipokea na Naamini tutashinda 🙏🏻.
No comments:
Post a Comment