Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mgeni rasmi maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama..Soma habari kamaili na matukio360..#share
Na Hussein Ndubikile
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yatakayofanyika kuanzia oktoba 16 hadi 21 mwaka huu katika Uwanja wa Mashujaa, mkoani Kilimanjaro.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
Hayo yamesemwa leo jjijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Hamad Masaun wakati akitoa taarifa kwa wanahabari kuhusu maadhimisho hayo.
Amesema Samia atayafungua maadhimsho hayo huku akisisitiza siku huyo itaendana na ukaguzi wa magari ya shule, abiria na mizigo na kwamba yatakayofanyiwa yatapatiwa stika maalum.
" Kama mnavyojua kila mwaka huwa tunaadhimisha wiki ya nenda kwa usalama mwaka Jana yalifanyika Dar es Salaam mwaka huu kitaifa yanafanyika Kilimanjaro yakiwa na Kauli mbiu isemayo zuia ajali tii sheria okoa maisha," amesema Massaun.
Amebainisha kuwa ukaguzi magari binafsi utafanyika baada ya kumalizika ukaguzi wa magari yaliyoainishwa na kwamba madereva watakaobainika kutokuwa na stika wamiliki watachukiliwa hatua kali za kisheria.
Amesisitiza kuwa hawataruhusu ugawaji holela wa stika kama miaka iliyopita uliokuwa ukifanywa na baadhi ya askari Wa kikosi cha usalama barabarani.
Pia amesema asilimia 70 ya ajali za barabarani zinatokana na makosa ya kibinadamu yakiwemo ya ulevi, uzembe na kutozingatia sheria za barabarani.
Aidha, amesema sheria zilizopo zina udhaifu mkubwa unaochangia kushindwa kudhibiti madereva wazembe na kwamba kuna mpango wa kuzifanyia marekebisho.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Kampuni ya Geita Gold Mine nchini, Simon Shayo amesema usalama wa raia barabarani ni muhimu na kwamba kampuni hiyo imetoa sh milioni 72 ili kufanikisha wiki hiyo.
Naye Mkurugenzi wa Selcom, Benjamini Mpawo amesema kampuni yake imesaidia sh.milioni 50 katika kufanikisha maadhimisho .
Mkurugenzi wa mahusiano na mambo ya nje wa kampuni ya TBl, Amanda Walter amefafanua kampuni hiyo inaiasa Jamii kuacha kunywa pombe kupitiliza ili kuepukana na ajali.
Amanda amebainisha Tbl imetoa sh milioni 30 kwenye maadhimisho hayo.
No comments:
Post a Comment