Watumishi TIA wapandishwa kizimbani...Soma habari kamili na Matukio360..#share



WATUMISHI wawili wa Chuo cha Uhasibu (TIA) jijini Dar es Salaam, leo wamefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka mawili ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya bilioni moja.
Watuhumiwa hao ni Shaha Mussa Hanzuruni na Onesphory Ambangile Luhungu. A
kisoma hati ya mashtaka m
bele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba,
 wakili wa serikali kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) Leornad Swai amesema kuwa
 kati ya January Mosi 2012 na Desemba 30 2014, washtakiwa hao walitenda kosa la matumizi mabaya ya madaraka.

Imedaiwa, washtakiwa, walitumia vibaya madaraka yao kwa kutofuata taratibu za manunuzi katika ununuzi wa ardhi wa chuo hicho (TIA) kampasi uya Mwanza na kimsababishia Vedasto Lupungo kupata manufaa ya Sh.1,097,681,107./-

Katika shtaka la pili imedaiwa siku na mahali hapo washtakiwa hao kwa ridhaa zao na matendo yao waliisababishia TIA Hasara ya Sh. 1,097,681,107/- kwa kutokifuata sheria za manunuzi wakati wa kusaini mkataba wa ardhi Wa eneo la TIA kampasi ya Mwanza.

Kwa kuwa DPP ameipa mamlaka mahakama ya Kisutu kisikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi, washtakiwa walipata nafasi ya kijibu juu ya tuhuma hizo ambapo wote wamekana kutenda makosa hayo na mahakama ikawasomea masharti ya dhamana kwa kuwa kesi hiyo inadhaminika

Akisoma masharti ya dhamana, Hakimu Simba amewata washtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaoweka bondi ya milioni 250 kila mmoja, pia amemtaka mdhamini mmoja kati ya hao kuweka mahakamani pesa taslimu, milioni 250 au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha ambayo Ipo ndani ya mkoa wa DSM.

Pia wametakiwa kuwasilisha Pasi zao za kusafiria vilevile hawaruhusiwi kusafiri nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila ruhusa ya maandishi kutoka mahakamani hapo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search