Waziri Ummy atoa miezi sita wakuu wa shule kuanzisha madawati ya ulinzi wa watoto shuleni..soma habari kamili na matukio360..#share


WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ametoa miezi sita Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari nchini kuhakikisha wanaanzisha madawati ya ulinzi na usalama wa watoto ili kusikiliza matatizo ya wanafunzi hususani wa kike.


Waziri Ummy Mwalimu akizindua kampeni ya kitaifa ya kutokomeza mimba za utotoni yenye kauli mbiu isemayo:” "Najitambua Elimu ndio Mpango mzima".


Kauli hiyo Ummy ameitoa leo akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo Kitaifa imefanyika wilayani Tarime, mkoani Mara, amewasisitiza wakuu hao kutekeleza agizo hilo kwani dawati ni mahali  keleza matatizo yao.


Ameongeza kuwa suala la kumlinda mtoto wa kike ni jukumu la kila 



mmoja katika jamii na kuwapongeza wadau wa maendeleo ya watoto kwa 
jitihada zao na kushirikiana na Serikali kutoa elimu kwa wanajamii 
kuhusu madhara ya mimba za utotoni, ukeketaji na ukatili dhidi ya 
wanawake na watoto.
 

Waziri Ummy Mwalimu akibonyeza kitufe kuzindua ujumbe wa radio wa kampeni ya kutokomeza mimba za utotoni yenye kauli mbiu isemayo:” Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima” 

Waziri Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto, wadau na madereva bodaboda wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara muda mfupi baada ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika kitaifa wilayani Tarime mkoani Mara. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search