Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan afanya mazungumzo na Balozi wa Ireland..Soma habari kamili na Matukio360..#share


MAKAMU wa Rais wa  Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Balozi wa Ireland nchini Paul Sherlock, Ikulu jijini Dar Es Salaam.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Ireland nchini  Paul Sherlock alimtembelea Makamu wa Rais ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam.


Balozi alizungumzia masuala mbalimbali yakiwemo kuwawezesha wanawake katika nafasi za kisiasa, Masuala ya Mimba za utotoni  na namna ya kukabiliana na vifo wakati wa kujifungua.


Kwa upande wake Samia Suluhu Hassan aliiomba nchi ya Ireland kuendelea kusaidia Tanzania katika kutoa elimu ya uzazi ili kupunguza Vifo vya akina mama na watoto wakati wa kujifungua.



Wakati huo huo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amkutana na kuzungumza na Balozi wa Morocco nchini Mhe. Abdelilah Benryane mwenye makazi yake mjini Nairobi,Kenya.



Katika mazungumzo yao, Balozi wa Morocco alimpatia taarifa ya utekelezaji wa yote yaliokubaliwa wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco na kumueleza Makamu kwamba utekelezaji wa mambo hayo umefikia hatua nzuri.



Kwa upande wake Mheshimiwa Makamu wa Rais alimpongeza Balozi kwa kusimamia utekelezaji huo ndani ya muda mfupi.



Makamu wa Rais alimueleza Balozi huyo wa Morocco kuwa uhusiano uliopo kati ya nchi mbili hizi ni wa kudumu na utasaidia katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo katika nchi hizi.Mwisho Kabisa Makamu wa Rais alikutana na kuzungumza na Balozi wa Sausi Arabia Mhe. Mohammed Almalik .



Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Saudi Arabia Mohammed Almalik(kushoto) aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar Es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)



Makamu wa  Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Morocco Abdelilah Benryane (kushoto), Ikulu jijini Dar es salaam. 

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akipokea taarifa kutoka kwa Balozi wa Morocco  Abdelilah Benryane (kushoto), Ikulu jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya makamu wa Rais).

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search