Makonda atahadharisha wakazi Dar es salaam... soma habari kamili na matukio360..#share

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametoa tahadhari kwamba mvua kubwa zaidi zitanyesha Dar kuanzia tarehe 1 November.


“Hali hii ya mvua itaendelea kuwa kubwa zaidi na tumeambiwa na Wataalamu kwamba inakuja nyingine kubwa zaidi kuanzia tarehe moja hivyo tujihadhari”

Pamoja na tahadhari hiyo, Makonda ameligiza Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ kujenga daraja la muda (daraja la Malecela) ambalo liliharibiwa na mvua zilizonyesha.

“Nimewaagiza JWTZ watakuja kujenga daraja la muda ili magari yapite wakati TANROADS wakijipanga kwa ajili ya ujenzi wa muda mrefu kurudisha miundombinu kama inavyotakiwa”

‘Nafahamu kuna nyumba zaidi ya 200 ziko katika sehemu hatarishi Kinondoni, zile 190 zilizobomoka pia tuendelee kushirikiana na Wadau kuhakikisha tunapata hifadhi huku tukijipanga kuwa na sehemu salama zaidi”

“Kamati ya maafa ya Mkoa imefanya kazi nzuri toka jana kwa kuokoa Wananchi wengi kwenye maeneo tofauti na kwakweli bila wao tungekua na idadi kubwa ya watu waliokufa”

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search