BoT, NBS wamjibu Zitto...Soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Abraham Ntambara
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imekanusha taarifa zilizotolewa na Kiongozi wa Chama
cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kiogoma Mjini Zitto Kabwe kuhusu takwimu za pato
la taifa, ujazi wa fedha na mfumuko wa bei ambazo anadai zinatia mashaka.
Mkurugenzi wa Sera na Tafiti toka Benki Kuu, Johnson Nyella
(kushoto)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati
akikanusha taarifa za upotoshaji kuhusu takwimu za pato la taifa mapema hii leo
jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa toka Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS) Daniel Masolwa.
Wakizungumza kwa
pamoja na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam leo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ,
wamesema taarifa hizo ni za uongo, upotoshaji na kuwataka wananchi wazipuuze.
Hivi karibuni Zitto alidai kuwa na mashaka juu ya takwimu za
ukuaji wa pato la taifa na mfumko wa bei kwenye robo iliyoishia Juni, 2017 kuwa
ulipaswa kuwa asilimia 0.1 na siyo asilimia 5.7 kama ilivyochapishwa katika
ripoti ya robo ya mwaka ya Benki Kuu.
Mkurugenzi wa Sera na Tafiti kutoka BoT Johnson Nyella, amesema ukuaji wa asilimia 5.7 alioutaja kiongozi huyo
wa ACT-Wazalendo ulikuwa wa robo ya kwanza ya mwaka 2017 na siyo robo ya pili.
“Ripoti ya Benki Kuu aliyoitumia ilikuwa na takwimu za hadi robo
ya kwanza mwaka 2017, kwani ilichapishwa kabla ya takwimu za pato la taifa za
robo ya pili hazijatolewa na Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) . Ukuaji wa pato
halisi la taifa katika robo ya pili ya mwaka 2017 ulikuwa asilimia 7.8,”
amesema Nyella.
Aidha amedai kuwa Zitto amekokotoa
ukuaji wa pato la taifa anaodai kuwa sahihi kwa kuangalia tofauti kati ya
ongezeko la ujazi wa fedha (m) na mfumuko wa bei (p).
Kwa upende wake Meneja wa Takwimu za
Pato la Taifa (NBS) Daniel Msolwa, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa
NBS, amesema Zitto anatakiwa kufahamu kuwa takwimu za robo ya mwaka
hurekebishwa (revised) baada ya kupatikana kwa taarifa za kina za uzalishaji wa
bidhaa na huduma katika nchi ikiwa ni pamoja na vitabu vya mahesabu
vilivyokaguliwa.
Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa kutoka Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) Daniel Masolwa (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akikanusha taarifa za upotoshaji kuhusu takwimu za pato la taifa
mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Tafiti
toka Benki Kuu, Johnson Nyella
“Ni vema Zitto Kabwe akawa makini na
uchambuzi anaofanya na siyo kuupotosha umma kwa kutumia kichaka cha takwimu au
mjadala wa kufurahisha umma. Kama hana ufahamu ni bora angeuliza aelimishwe
kabla ya kuendelea na uchambuzi wake na hatimaye angeweza kuja na ripoti yenye
mashiko,” amesema Msolwa.
No comments:
Post a Comment