Matokeo Darasa la saba 2017 yatangazwa..Soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Abraham Ntambara
BARAZA la Mitihani nchini (NECTA) limesema kiwango cha ufaulu katika mtihani wa darasa la saba uliofanyika Septemba 6 hadi 7 mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 2.40 ukilinganisha na mwaka jana.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa NECTA Dk. Charles Msonde akitangaza matokeo hayo, amesema watahiniwa
662,035 kati ya 909,950 waliofanya mtihani wamefaulu kwa kupata alama 100 au Zaidi
kati ya alama 250.
Kati yao Wasichana ni
341,020 ambao ni sawa na asilimia 70.93 huku wavulana ni 321,015 sawa na asilimia 74.80.
Dk. Msonde amesema pia katika takwimu za matokeo zinaonyesha
ufahulu katika masomo ya Kiswahili,Kiingereza
na Hisabati umepanda kwa asilimia
4.25 ikilinganishwa
na mwaka 2016.
“Watahiniwa wamefaulu Zaidi
katika somo la Kiswahili ambapo ufaulu ni asilimia 86.86 na somo walilofaulu
kwa kiwango cha chini Zaidi ni English Language lenye ufaulu wa asilimia 40.30,”amesema Dkt Msonde.
Hata hivyo Dk. Msonde ameiitaja mikoa iliyoongoza kitaifa ni
Dar eSalaam,Geita,Kagera,Iringa,Kilimanjaro,Njombe, Arusha, Mwanza, Katavi, Tabora.
Kuhusu wanafunzi 10 bora kitaifa waliofanya vizuri kwenye mtihani
huo ni Ibrahim Shaban kutoka Shule ya Tusiime iliyopo mkoani Dar es Salaam,
Kadidi Mkama Kaddi kutoka shule ya Paradise iliyopo mkoani Geita,Mahir Ally Muhamed
kutoka shule Feza iliyopo Mkoani Dar es Salaam,Mbarak Faraj kutoka shule hiyo
hiyo ya Feza,
Dk, Msonde amewataja wengine waliofanya vizuri ni Philimon
Damas kutoka shule ya St.Achileus
iliyopo mkoani Kagera ,Huruma Godfrey kutoka shule Mwanga iliyopo Mkoani Kagera ,Hamza Azael
Almas kutoka shule ya Azina iliyopo
Mkoani Dar es Salaam,Gibbons Roy
Fountain of Joy iliyopo Dar es Salaam,pamoja Erastus Joseph kutoka shule St Peter Claver iliyopo Mkoani Kagera.
Pamoja na hayo Dk Msonde Baraza hilo limetoa wito kwa
Maafisa elimu wa Mkoa
,Halmashauri,Manispaa ,wadhibiti Ubora wa Elimu,wamiliki wa shule,Walimu
wahakikishe ufundishaji na ujifunzaji unaimarishwa katika
masomo yote shuleni ili kuwawezesha wanafunzi kupata umahiri
unaotarajiwa.
No comments:
Post a Comment