Mauaji Kanumba ushahidi waendelea kutolewa dhidi ya Lulu...Soma habari kamili na Matukio360

Na Mwandishi Wetu

DR. PAPLAS Kagaiya (35) amedai aliondoka na kumuacha Steven Kanumba peke yake baada ya kuanguka.
Mwigizaji wa Filamu Elizabeth Michael 'Lulu'

Dk. Kagaiya ambaye ni shahidi wa pili katika kesi ya mauaji ya bila kukusudia inayomkabili mwigizaji Elizabeth Michael 'Lulu' ameieleza Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam leo kuwa aligundua Kanumba amekufa alivyomfanyia vipimo.

Amedai hayo mbele ya Jaji Sam Rugamanyika wakati akitoa ushahidi wake kuwa alimpima presha na sukari ambapo sukari ilikuwa sawa lakin mapigo ya moyo hayakuepo kabisa.

"Nilijua ameshakufa  akiwa pale nyumbani kwake ila sikutaka kuwaambia paka daktari mwingine athibitishe"alidai

Akiongozwa na wakili wa Serikali Batilda Mushi Kagaiya alidai baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mdogo wa marehemu Seth Bosco alimfuata alimfuata Hospitalini kwake St. Anna  Manzese na kurudi nae Sinza ambapo aliondoka na vifaa.

Paplas ambaye pia ni Daktari wa familia ya Marehemu Kanumba alipata elimu yake ya Advance Diploma Chuo cha Udaktari cha jeshi Lugalo na kwamba aliitibu familia hiyo kwa mika kati ya mitano na sita

Alidai Aprili 7,2012 alikuwa ofisini kwake ambapo alipigiwa simu na Seth Bosco akamuangalie Kanumba amedondoka ambapo alichukua vifaa ikiwemo BP Mashine

Aliendelea alipofika nyumbani kwake hakumkuta mtu mwingine ambapo alimkuta Kanumba kalala chini akampima presha na sukari baada ya hapo alimwambia Seth amvalishe nguo wampeleke hospitali kubwa kama Muhimbili akafanyiwe vipimo.

Alidai aliondika na Seth kaka mwingine ambaye alikwenda kuwasaidia ambapo pia waliongozana na mama mwenyenyumba  walipofika Muhimbili walimpeleka Emergence ambapo Daktari alimpima akasema ameshafariki

"Hata ndani hatukumuingiza alipimwa palepale tukaambiwa amefariki na niliambiwe niende Salenda bridge nikachukue PF 3 na nilivyorudi walinipa askari tukaupeleka mwili Mochuari"alidai.

Alidai baada ya hapo walienda kituo cha polis Ostarbay kwaajili ya mahojiano ambapo alidai kuwa alikuwa akimtibu kanumba magonjwa mbalimbali ikiwemo Malaria na mafua.

Alipoulizwa kama anamfahamu  Elizabeth Michael alijibu anamfahamu kupitia kanumba na kwamba alikuwa mpenzi wake.
"Tulivyotoka polis kwaajili ya mahojiano  nikikuwa na polisi ambapo nilikuwa nampigia simu nikamwambia tukutane Bamaga"

Aliulizwa na Walikili wa utetezi Peter Kibatala alimuuliza kama aliwahi kumfanyia vipimo kama anauvimbe kwenye ubongo akajibu hakuwahi kumfanyia uchunguzi kama anauvimbe kichwani.

Alipoulizwa kanini alipofika alimpima sukari alijibu, mtu akianguka ghafla inawezekana sukari ilikuwa chini ndio maana akadondoka.

Kabla ya tarehe 7, alidai hakuwahi kumpima hakuwahi kumfanyia uchunguzi kuhusu sukari na kwamba hakujua ni nani alimlaza  Kanumba chali.

Alidai hakuangalia kama kitanda cha marehemu kilikuwa kimevurugika na hajui kama kulikuwa na pombe chumbani pamoja na kwamba hakutambua kama amekunywa kilevi.

Pia alidai marehemu hakumkuta na jeraha lolote na kwamba mshtakiwa alikuwa akimpigia simu mara kwa mara kujua hali ya marehemu na kwamba alijua marehemu alikuwa amezimia.

"Pia Lulu alikuwa na hofu kwamba marehemu ameshakufa, mmi nilimwambia tukutane bamaga na alikuwa hajui kama kanumba amekufa"alidai.

Kwa upande wake,Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi,Mkoa wa Kipolisi Kinondoni,Kituo cha polis Oyestebay Ester Zephania aliieleza mahakama hiyo kuwa,  baadhi ya wasanii akiwamo ray na Dk Paplas walifika kituo cha Polisi Oysterbay kwa ajili ya kutoa taarifa za kifo cha marehemu Kanumba.

Aliieleza kuwa, Mara baada ya kutolewa kwa taarifa hizo,Mkuu wa upelelezi wa Polisi Mkoa wa Kinondoni wakati huo alikua Kamanda Camillus Wambura alimtuma kwenda yeye pamoja na askari wengine wawili  nyumbani kwa Kanumba kwa ajili ya kufuatilia kilichotokea.

Aliieleza kuwa, walipofika nyumbani hapo muda wa saa tisa usiku, walikuta watu wamejaa huku wengine wanalia,ndipo walipoonyeshwa mdogo wa marehemu Kanumba aliyejitambulisha kuwa jina la Seth Bosco ambaye waliongea nae na kuwapeleka chumbani kwa Kanumba.

Aliieleza walipoingia ndani walianza ukaguzi ambapo uvunguni mwa kitanda walikuta panga,pembeni mwa kitanda walikuta stuli iliyokua na chupa ya sprite,pombe aina ya jack Daniel pamoja na glasi iliyokuwa na  kinywaji ambacho hawakukitambua pamoja na michirizi meusi ukutani

Aliieleza kuwa, Mara baada ya kuona hivyo vitu,aliwasiliana na afande wambura ambaye aliwaambia wasiondoke mpaka watakapofika wapelelezi wengine ambao maarufu kama nyota tatu ili waweze kufanya uchunguzi zaidi wa tukio hilo.

Aliieleza kuwa, baadae ya hapo,,afande wambura alimwambia warudi ofisini na kuandika Maelezo ya walichokiona lakini wahakikishe  wanampata Lulu kwa ajili ya kuwasaidia katika upelelezi .

Aliieleza kuwa, kutokana na hali hiyo, afande Wambura aliwakabidhi Dk Paplas na kuwaambia kuwa Dk huyo amekua akiwasiliana na Lulu Mara kwa Mara.

Aliieleza kuwa, kutokana na hali hiyo, walimwambia Dk Paplas awasiliane na lulu ili waweze kujua namna ya kumpata ambapo Dk huyo aliwasiliana na Lulu na kumwambia waonane Bamaga .

"Tuliondoka na Dk Paplas hadi bamaga ,tulipofika sisi tulikaa pembeni na Dk alikaa upande mwingine.Baadae ikaja gari ndani yake kulikua na dereva na Lulu,  Dk Paplas aliinuka na kwenda kwenye gari hilo na walipofika mlangoni lulu alishuka kwenye gari wakawa wanaongea na Dk, nikajitokeza na kujitambulisha kama ni askari natoka kituo cha Polisi Oysterbay upo chini ya ulinzi,"aliieleza.

Alieleza kuwa,walimchukua Lulu hadi kituo cha Polisi Oysterbay na kumkabidhi kwa afande wa wambura,Mara baada ya kumkabidhi, kilichotokea hajui lakni baadae aliitwa na kuambiwa ampeleke lulu hospitali kwa sababu alidai ana maumivu mwilini.

Aliieleza,walikwenda hadi hospitality na kuonana na dakati lakini alikua hajui anaumwa nini kwa sababu hajaingia ndani ya cha mahojiano na daktari.

Aliieleza baada ya hapo alimrudisha lulu Polisi Oysterbay na kumkabidhi kwa afande wambura.

Baada ya ushahidi huo Jaji Rumanyika aliahirisha kesi hiyo hadi Octobar 23 kwaajili ya kuendelea na shahidi mmoja aliyepakia.

Kwa upande wake wakili Kibatala alimuuliza kuwa  lulu alikuwa amepigwa na mapanga mapajani akajibu hakumwambia na kwamba hakuona majeraha ya lulu.

Alimuuliza kama walichukua maele za Dr aliyemtibu lulu akajibu hapana na daktari yuyo hakumpa majibu ya alichompima

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search