Mauaji Kanumba ushahidi waanza kutolewa dhidi ya Lulu...soma habari kamili na Matukio360...#share
Na Mwandishi wetu
SETH Bosco(30)
amedai muigizaji
Elizabeth Michael 'Lulu' aliondoka na kumuacha Steven Kanumba peke yake baada
ya kuanguka
Elizabeth Michael maarufu Lulu
Bosco ambaye
ni mdogo wa marehemu Kanumba amesema hayo leo jijini Dar es Salaam katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar
es Salaam, mbele ya Jaji Sam Rumanyika wakati akitoa ushahidi wake
Shahidi huyo
wa kwanza wa upande wa mashtaka kwa kesi hiyo ya mauaji ya bila kukusudia amedai licha ya kumweleza Lulu abaki na Kanumba,
yeye alipomfuata daktari aliondoka na kumuacha peke yake.
Awali Lulu alikumbushiwa
mashtaka yake ya kwamba April, 2012 huko
Sinza Vatican wilayani Kinondoni alimuua bila kukusidia Kanumba, Lulu alikana
shtaka hilo.
Akiongozwa na
Wakili wa serikali Faraja George, Bosco
amedai baada ya kupata taarifa za kudondoka kwa Kanumba kutoka kwa Lulu
alimpigia simu daktari wao aliyemtaja kwa jina la Paplas ambaye alimtaka kwenda
kumchukua Hospitalini kwake na kwa kuwa hakukuwa na usafiri aliwasha gari na
kumfuata na kumuomba Lulu abaki na Kanumba.
"Wakati
narudi na Dokta, Lulu alinipigia simu akasema nimemuwekea maji kifuani Kanumba lakini haamki nikamwambia nisubiri lakini nilipofika
sikumkuta" amesema
Alidai baada
ya Dokta kufika na kumpima alishauri apelekwe Muhimbili, kwa msaada wa jirani aliyemtaja kwa jina la Baraka walimbeba
Kanumba na kumuingiza kwenye gari hadi Muhimbili.
Alidai wakati
wanaangaika kumuingiza Kanumba kwenye gari, mama mwenye nyumba alisikia
akafungua mlango aliposikia tatizo nae aliwasha gari lake na kuwasindikiza,
ambapo walienda moja kwa moja Emergency na baada kumfanyia Kanumba uchunguzi
Dokta aliwaambia amefariki na watafute taratibu za polisi
Amedai walienda Kituo cha Polisi Urafiki, wakiwa huko
Lulu alikuwa akimpigia Dk Paplas simu ndipo polisi wakamuomba Dokta aweze
kuwasaidia kumpata Lulu ambapo asubuhi
ya Aprili 7, baada ya wao kumaliza kuhojiwa Lulu alakamatwa.
Akielezea
jinsi tukio hilo alidai, Aprili 4 mwaka
2012 alishinda nyumbani na kaka yake toka asubuhi na ilipofika mida ya saa kumi
jioni, Kanumba alimuomba asitoke na wangetoka pamoja usiku wa saa sita.
Alidai
ilipofika Saa sita kasoro za usiku Kanumba alimwambia wajiandae watoke, ambapo
yeye alikuwa wa Kwanza kumaliza kujiandaa lakini alipotoka chumbani kwake
akielekea sebuleni, alikutana na Kanumba akipita kwenye koridoni huku akiwa
amevalia taulo kuelekea sebuleni, akipaka Mafuta kichwani na kwamba sebuleni
kwa nje kulikuwa na Gari la Lulu.
Alidai kuwa,
Kanumba ndiye alimfungulia mlango lulu, waliingia wote ndani akiwa chumbani
kwake ambako alirudi kumsubiria Kanumba huku mlango wake ukiwa wazi kidogo,
wakati wakitembea Koridoni kuelekea chumbani kwa Kanumba alisikia wakigombana huku Kanumba
akimuuliza lulu kwa nini anaongea na boyfriend wake mbele yake.
Aliendelea
kudai kuwa muda wote huo walikuwa wakivutana, Lulu akitaka kutoka nje na
Kanumba akimvutia ndani mara waliingia chumbani na mlango ukafungwa.
"
Nilisikia sauti za kupigana na muda mfupi kidogo Lulu alifungua mlango na kuja
chumbani kwangu akasema, Kanumba amedondoka sijui amekuwaje"alidai
Alidai
aliondoka hadi chumbani kwake, alimkuta Kanumba amedondoka kwa kuegemea ukuta
huku akiwa hawezi kupumua, (amesafocate), alimchukua na kumlaza chini kisha
akampigia simu Dr Paplas na Mazingira ya
chumba hicho cha kaka yake yalikuwa ya kawaida kama siku zote.
Alidai baada
ya hapo aliwasha gari na kwenda
kumchukua Dr ndipo Lulu akanipogia simu na kusema Kanumba haamki.
Wakili wa
utetezi, Peter Kibatala alimuuliza Shahidi kama ushahidi aliotoa mahakamani
unafanana na maelezo waliyoyatoa polis
ambapo alijibu ndio.
Kibatala
alimuuliza shahidi huyo ni wapi aliwaeleza polisi kuwa alimuacha mshtakiwa Lulu
peke yake na Marehemu Kanumba wakati anaenda kumtafuta Dr, Paplas alisem
hakuwaeleza.
Alidai kuwa
yeye alikuwepo kwenye postmotam ya kawaida na wala hakuwepo wakati wakichukua
sampuli za mwili kupeleka maabara.
Jaji Manyika
aliarisha kesi hiyo hadi leo ambapo itaendelea na ushahidi wa Dr Paplas ambaye
jana alishindwa kutoa ushahidi kwasababu alikuwa hajiskii vizuri
February
18/2014 akisomewa maelezo ya awali, Lulu
alikiri mahakamani kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kanumba na pia kuwa
kulikuwepo na ugomvi baina yao siku ya tukio la kifo cha mwigizaji huyo.
Kwa mara ya
kwanza Lulu alipandishwa kizimbani Aprili 11,2012 mbele ya Hakimu mfawidhi wa wakati huo wa Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, Augustina Mbando
ambapo alisomewa mashitaka ya mauaji.
Lulu aliachiwa
kwa dhamana Januari 29, 2013 baada ya kesi hiyo kubadilishwa hati ya mashitaka
kutoka kwenye kesi ya mauaji kwenda mauaji ya bila kukusudia ambapo badiliko hilo
lilimpa nafasi ya kupata dhamana.
Katika kesi ya
msingi namba 125 ya mwaka 2012, inadaiwa kuwa Aprili 7, 2012 Sinza Vatican jijini Dar es Salaam, Lulu
alimuua Kanumba bila kukusudia.
No comments:
Post a Comment