Zitto azidi kukimbiwa, Mwingamba wenzake 10 wajiunga CCM..soma habari kamili na Matukio360..#share
Na Abraham Ntambara
ALIYEKUWA Mwenyekiti
wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi Taifa ya Chama Cha ACT Wazalendo Samson
Mwigamba na wenzake 10 wamejiunga na CCM.
Samson Mwigamba na baadhi wa wanaACT-Wazalendo Leo jijini Dar es Salaam wakitangaza kujiunga na CCM
Hatua hiyo inakuja ikiwa
ni siku chache Mwigamba kung'atuka nafasi yake hiyo katika chama hicho na kudai
angebaki kuwa mwananchama wa kawaida akidai kuna mambo ndani ya chama hicho
hayaendi sawa.
Mwigamba alidai alijitahidi
kuongea na viongozi wakuu wa chama hicho
kuhusu mambo mbalimbali lakini hayatendeki wala kufanyiwa kazi hivyo kufanya
maamuzi hayo ili kutopingana nao na aweze kupata nafasi ya kuhoji baadhi ya
mambo ndani ya chama
Lakini leo jijini Dar
es Salaam katika mkutano wake na waandishi habari ametanga kujiunga na CCM na
kwamba wana ACT-Wazalendo zaidi ya kumi nao wameng’atuka kutoka chama hicho.
Viongozi hao waliotangaza
kukihama chama hicho ni Wilfred Kitumba
mwenyekiti wa Act-Wazalendo mkoan Singida, Liploth Robert Katibu wa Chama hicho mkoani Singida, Emmanuel
Wilfred ofisa utawala chama cha
Act-wazalendo Makao makuu.
Wengine ni Mwamtumu Mgonjwa ambaye ni ofisa wa Sheria wa
chama hicho Taifa, Peter Mwambeja mtunza
hazina wa Chama, Dasan Ullotu ambaye ni Katibu wa Chama Mkoani Arusha, Wilson
Laizer Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Arusha.
Wengine ni Nakamia
Wazael ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho jimbo la Singida Mjini, na Denson
Chembo Katibu wa chama uadalifu Taifa.
Miongoni mwa sababu
za kujiondoa kwao ni kuwa chama kimekosa dira na uelekeo na kimekuwa ni cha
uanaharakati.
“Kwa sasa tumeamua
kung’atuka ACT-Wazalendo na tunajiunga CCM kwa kuwa kinaanza kutekeleza misingi
ya Azimio la Arusha ambalo sisi ndio ilikuwa dira yetu,” amesema Mwantumu.
No comments:
Post a Comment