Mauzo ya hisa DSE yashuka...soma habari kamili na Matukio360..#share

Salha Mohamed
THAMANI ya mauzo ya hisa katika soko la hisa Dar es Salaam (DSE),imepungua kutoka bilioni 30 Oktoba 13 hadi  bilioni 23,  Oktoba 20, 2017.


Afisa mwandamizi wa masoko DSE, Mary Kinabo Hata hivyo Ofisa Mwandamizi wa masoko DSE, Mary Kinabo amesema "Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepanda kutoka hisa milioni 2.5 ya Oktoba 13, 2017 hadi hisa mil 2.8 kwa Oktoba 23, 2017."

Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa ni kampuni ya Bia (TBL) kwa asilimia 89, Kiwanda cha Sigara(TCC) asilimia kumi, na Benki ya  CRDB asilimia moja.

Kinabo ameongeza kuwa ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika soko umepanda kwa bilioni 463 kutoka trilioni 20.4 kwa wiki iliyopita hadi  trilioni 20.9 hadi Oktoba 23, 2017.

"Ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umeongezeka kwa  bilioni 205 kutoka trilioni 9.96 hadi kafika trilioni 10.2 wiki hii...hii ni kutokana na  kupanda kwa bei ya hisa za  TCC kwa asilimia saba, TBL asilimia tatu na DSE kwa asilimia mbili. 

Ameongeza kuwa kiashiria cha kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko (DSEI) kimepanda kwa pointi 48 kutoka pointi 2,124 hadi 2,172 kufikia pointi kutokana na kupanda kwa bei za hisa za Uchumi Supermarket Ltd (USL) kampuni Kenya Airways (KA) na Acacia (ACA).

Amesema kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) kimepanda kwa pointi 193 kutoka pointi 5,187 hadi pointi 5,380 huku kiashiria cha huduma za kibenki na kifedha  (BI) kimeshuka kwa pointi 16 kutoka pointi 2514 hadi pointi 2498.


Kinabo amesema mauzo ya hati fungani Oktoba 20, 2017 yalikuwa Sh. bilioni 13 kutoka Sh. bilioni 9 hadi Octoba 13 mwaka huu yametokana na hatifungani 21 za serikali na mashirika binafsi zenye jumla ya thamani ya Sh. bilioni 23 kwa jumla ya gharama ya Sh. bilioni 13.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search