Mawaziri, Wabunge kugombea tuzo...soma habari kamili na Matukio360...#share
Na Salha Mohamed
KAMATI ya utawala ya shinadano la tuzo za utekelezaji maendeleo kwa kasi ya juu kwa Wabunge na Mawaziri (THSDA)
imezindua shindano la kutoa tuzo kwa wabunge na mawaziri watakaofanya vizuri
katika kutekeleza majukumu yao na kuwaletea wananchi maendeleo.
Mkurugenzi mkuu wa THSDA, Herman Mnenuka wa pili kutoka kushota akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
Lengo la tuzo hizo ni kupima utekelezaji wa shughuli za huduma na maendeleo kwa wananchi.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Katibu wa Kamati hiyo Wilson
Maage amesema tuzo hizo zitapima kasi za shughuli za vingozi wa ngazi
mbalimbali katika sekta na taasisi za kiserikali na taasisi hapa nchini.
“Tuzo hizo zimetokana na kuwepo
wazo bunifu (intellectual property) ambalo azma yake ni kuhamasisha utekelezaji
wa shughuli za huduma na maendeleo kwa wananchi wa Tanzania na kupima kasi ya
utekelezaji wa shughuli hizo kwa viongozi wa ngazi mbalimbali katika sekta na
taasisi za kiserikali hapa nchini,” amesema.
Amesema kufanyika kwa tuzo hizo ni
kuwaweka wananchi karibu na viongozi, kuchochea utekelezaji huduma na
maendeleo kwa kasi ya juu, utawla bora na uwajibikaji wa viongozi kwa Wananchi,
uhusiano mzuri kati ya serikali na Wananchi na kuimarisha furaha, utulivu na
amani.
Amefafanua kuwa wahusika katika
shindan hilo ni wabunge pamoja na Mawaziri ambaye ni mtetezi wa wananchi wake
bila uoga akiwa ndani au nje ya Bunge.
“Sifa zingine ni awe mtendaji bora
wa maendeleo yenye kuonekana, sifa ya kutoa hoja zenye tija kwa kutumia lugha
ya staha bila matusi, sifa ya utekelezaji wa haraka apatapo matatizo ya
Wananchi wake pamoja na sifa ya kutetea demokrasia, uhuru na kutetea wanyonge.
Mkurugenzi Mkuu wa Kamati hiyo, Herman
Mnenuka amesema kuwa wananchi ndiyo nguzo kuu ya kupata kiongozi atakayepata
tuzo hiyo kwani wao ndio watakaopendekeza majina ya wabunge pamoja na wamaziri
wanaofaa kuwania tuzo hiyo.
Tuzo hizo ni za kwanza kutolewa hapa nchini na zitafika
tamati Desemba 23 mwaka huu ambapo wananchi wanapaswa kupendekeza
wabunge 15 kwa kila kigezo shindanishi, pia Wananchi watawateua Mawaziri 5 kwa
kila kipengele shindanishi kwaajili ya kuingia kwenye ushindani wa tuzo hiyo na
wabunge watano na Mawaziri watatu watakaopata kura nyingi kwa njia ya ujumbe
mfupi (SMS) kutoka kwa wananchi wataingia katika fainali ya king’anyiro kuwania
tuzo hiyo.
No comments:
Post a Comment