Mbunge Msigwa amuamshia dude Spika Ndugai...Soma habari kamili na Matukio360...#share
MBUNGE wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Mchungaji Peter Msigwa amesema anakusudia kupeleka hoja
binafsi katika bunge lijalo ya kumuondoa
Spika wa Bunge Jobu Ndugai.
Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa (kushoto) na Spika wa Bunge Job Ndugai (Kulia).
Amesema hayo leo kupitia moja ya mtanadao wake wa kijamii na
kubainisha kuwa atapeleka hoja hiyo kwenye bunge linalotarajia kuanza Novemba 7
mwaka huu.
Msigwa amefafanua kwa kusema kuwa atafanya hivyo kwa
kuzingatia kanuni ya 137 ya kanuni za kudumu za Bunge.
"Ninakusudia kupeleka hoja ya kumuondoa Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Job Ndungai, kwa kuzingatia Kanuni ya 137
ya kanuni za kudumu za bunge ina complement ibara ya 84 (7) (d) ya Katiba"
amesema Msigwa.
Mbunge huyo ni mmoja kati ya wabunge wa upinzani ambao
wamekuwa wakilalamika Spika Ndugai kwa kudai kuwa analiendesha bunge kwa
shinikizo na upendeleo, hivyo kudai kuwa hastahili kuendelea kuongoza kiti
hicho.
No comments:
Post a Comment