Mechi Simba, Yanga Polisi watahadhalisha...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
Salha Mohamed
JESHI
la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, linawataka mashabiki wasiokuwa na
tiketi kutofika uwanjani ili kuepusha usumbufu watakaoupata katika mechi ya
Ligi Kuu kati ya Simba na Yanga.
Kamanda wa Polisi, Lazaro Mambosasa
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kanda hiyo SACP, Lazaro
Mambosasa amesema mechi hiyo inachezwa leo katika Uwanja wa Uhuru’ shamba la
bibi’. ameahidi usalama wa kutosha katika mechi hiyo.
Amesema
wananchi wasiwe na wasiwasi wa kiusalama na kupaswa kutoa ushirikiano kwa kutoa
taarifa kwa jambo lolote watakaloliona kuwa linaweza kuwa chanzo cha uvunjifu
wa amani kwa kipindi chote watakapokuwa ndani au nje ya uwanja.
“Mashabiki
wanatakiwa kuwahi mapema ili kuepuka usumbufu unaoweza kutokea, tiketi
hazitauzwa siku ya mechi hivyo mashabiki wanatakiwa kukata tiketi
mapema,”amesema.
Amesema
tiketi 23,000 zitauzwa kutokana na uwezo wa uwanja huo, hivyo kwa wale
mashabiki watakaochelewa kukata tiketi wanashauriwa kuangalia mechi hiyo
kupitia Television na kusikiliza Radio.
Amesema
mashabiki wa pande zote mbili wanatakiwa kukaa katika sehemu zao maalumu
watakazopangiwa huku akibainisha uwepo wa askari wa kutosha ili kuhakikisha
sehemu zote za mageti ya kuingilia watu wanapekuliwa na magari hayataruhusiwa
kuingia ndani ya uwanja bali watu wanatakiwa kuyapaki nje ya uwanja.
“Pamoja
na hayo wananchi wanatakiwa kuwa watulivu katika kushangilia mechi hiyo, na
kuepuka kuingia na chupa za maji, kuingia na mabegi, kuingia na silaha ya aina
yoyote, kupaki magari ndani ya uwanja kukaa sehemu ambazo tiketi zao
haziwaruhusu,”amesema Mambosasa.
No comments:
Post a Comment