Zitto kujibu mapigo kwa rais Magufuli..soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
Mwandishi wetu
CHAMA
cha ACT Wazalendo leo kinatarajia kutoa hadharani taarifa ya kamati kuu ya
chama hicho kuhusu Takwimu za pato la taifa.
Kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe
Takwimu
hizo zitatangazwa na kiongozi mkuu wa
ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye pia ni mbunge wa Kigoma mjini
Afisa
habari wa ACT Wazalendo Abdallah Khamis amesema ‘Leo Oktoba 28, 2017, Kiongozi
wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe atazungumza na Waandishi wa
Habari kuhusu Taarifa ya Kamati Kuu ya Chama juu ya Takwimu za Pato la Taifa.’
Hatua
hiyo inaaelezwa kuwa ni kujibu mapigo kwa rais Dk John Magufuli ambaye hivi
karibuni alipokuwa akiwatunuku tuzo ya shukran wajumbe wa kamati za madini ya
almasi, dhahabu na Tanzanite.
Katika
hafla hiyo rais Magufuli alimtaka waziri wa Katiba Profesa Paramangamba Kabudi
kuhakikisha sheria ya Takwimu inafanya kazi ili kudhibiti na kuwachukulia hatua
za kisheria wote wanaotoa takwimu ambazo si sahihi.
No comments:
Post a Comment