Mkurugenzi LHRC Dk. Kijo Bisimba Amtembelea Tundu Lissu.. Ashangazwa na Kauli Hii Toka Kwa Lissu Baada ya Kumuona...#share


iMKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dkt Helen Kijo Bisimba (Pichani)leo amesafiri mpaka Nairobi nchini Kenya kwenda kumjulia hali Mbunge Singida Mashariki, Tundu Lissu. ambapo anapatiwa matibabu baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana Mjini Dodoma.
Mwanaharakati huyu maarufu nchini ,katika safari yake hiyo , aliongozana  na watetezi wenzake na haki za Binadamu ambapo  mara baada ya kumjulia hali Lissu ambaye ni Rais wa chama cha wanasheria nchini,(TLS) , amesema haya

"Leo Mungu amenipa neema kumuona Mh. Tundu Antipas Mughway Lissu nimeuona kwa macho muujiza kuwa Tundu pamoja na marisasi yale yote ameniona na kuniamkia nakunipa pole. Yaani yeye ndio anatupa sisi moyo kuwa Kufa mtu hufa mara moja tusiogope kusimamia haki, "


Pichani ni Mkurugenzi wa (LHRC)Dk Bisimba akiwa na watetezi wenzange mjini Nairobi Kenya



Ameongeza kusema kuwa "kusema ukweli, kutetea wanaoonewa.Nimepata nguvu mpya.Watanzania Tundu anawasalimu. Nimemuona anabariki.Mke wake mpenzi naye anaendelea na huduma kwa moyo mkuu ndiye niliye naye pichani.Waliotenda tendo lile wamrudie Mungu maana yupo tena yu hai na amewaonyesha ukuu wake. Mungu akamilishe uponyaji kwa Lissu."Amesema Dk Bisimba

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search