Waziri Kairuki: Watumishi hewa walininyima usingizi..Soma habari kamili na Matukio360..#share

Na Abraham
Ntambara
WAZIRI wa Madini Angella Kairuki amesema suala la uhakiki wa watumishi hewa lilimnyima usingizi katika kipindi alichokuwa Waziri wa Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora.
Waziri wa Madini Angella Kairuki akimkabidhi Kitendea kazi Waziri Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika jijini Dar es Salaam.
Kairuki amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati
akimkabidhi ofisi Waziri Mpya wa Ofisi ya Rais –Utumishi na Utawala Bora George
Mkuchika, amebainisha kuwa ni kutokana na baadha ya Maafisa Utumishi kutokuwa waaminifu
kwa kutoa taarifa zisizo sahihi za watumishi.
“Changamoto kubwa niliyokabiliana nayo ni suala la
uhakiki wa watumishi, suala kubwa ni baadhi ya Maafisa Utumishi hawakuwa
waaminifu katika kutoa taarifa sahihi,” amesema Waziri Kairuki.
Aidha amesema kuwa kwa kipindi chote cha miezi 23 alichokuwa
waziri wa Utumishi alikuwa akitengeneza mazingira mazuru kwa kurekebisha na
kurejesha nidhamu ya watumishi wa umma katika kutumikia wananchi.
Katika zoezi la uhakiki wa watumishi hewa lililofanywa
nchini, zaidi ya watumishi 10295 walibainika kutokuwa na sifa za kuwa
watumisshi wa umma.
Kwa upande wake Waziri Mkuchika amesema katika kipindi
chake cha kuiongoza wizara hiyo hatavumilia watumishi wazembe watakaoshindwa
kukaa mahali pao pakazi muda wa masaa ya kazi ili kuwatumikia wananchi kwa
kisingizio cha kwenda mjini kunywa chai.
“Nitahakikisha
watumishi wanawatumikia wananchi kwa nidhamu na mambo ya kizebe sitayakubali,
nataka watumishi walipwe mishahara kamili kwa kazi kamili,” amesema Mkuchika.
Amebainisha kuwa watumishi wamekuwa wakilipwa
mishahara kamili kwa kazi nusu kwani wamekuwa hawakai ofisini huku akiwataka
kutumia kantini zao kwa masuala ya chakula au kutafuta utaratibu mwengine
lakini siyo nje ya ofisi.
Katika mwaka wa fedha wa mwaka huu, amesema katika
kuboresha maslahi ya watumishi, zaidi ya watumishi 20,0000 watapandishwa
madaraja na vyeo.
Aidha amesisitiza kuwa ili kupiga vita suala la rusha wizara
yake itahakikisha inatoa elimu ya rushwa kawa wananchi kwani wamekuwa wakitoa
rushwa kwa kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya masuala hayo.

Waziri wa Madidi Angella Kairuki na Waziri wa Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora George Mkuchika Wakizungumza na waandishi wa habari wakati wa makabidhiano ya ofisi leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment