Polisi: Tunamshikilia Kigaila Benson wa Chadema..Soma habari kamili na Matukio360
Na Salha Mohamed
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limemshikilia
Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo(Chadema), Kigaila Benson kwa madai ya kutoa
lugha za uchochezi na za kashfa.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Lazaro Mambosasa.
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, SACP Lazaro Mambosasa
amethibitisha kukamatwa kwa Mkurugenzi huyo kwa mahojiano kwa madai ya
kutoa lugha za kuikashfu serikali na watu wake.
Amesema"Tunaendelea kumshikilia na anaendelea kuhijiwa
atakapokamilisha yale ambayo anamuhusu tutaelekeza kesi mahakamani kama
ushahidi utakuwepo wa kutosha,"amesema.
Mambosasa amesema endapo ushahidi utakuwa wa kuendelea na
mashahidi wengine wataangalia kupata dhamana huko mbele kwani jeshi
hilo halijakamilisha yale waliokusudia.
"Tunaendelea na upelelezi na tukimaliza tutalileta kwenu
kuwaambia hatua gani tumezichukua,"amesema.
No comments:
Post a Comment