Samia Suluhu aipa neno UN...soma habari kamili na Matukio360...#share

Na Hussein Ndubikila
SERIKALI imeiomba Umoja wa Mataifa(UN) kusaidia kufanikisha malengo ya Tanzania kufikia nchi ya uchumi wa viwanda vya kati ifikapo mwaka 2025.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipata salamu ya heshima toka kwa gwaride maalum la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (hawapo pichani) wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 72 toka kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Imebainisha kuwa mwaka 2016 sekta ya viwanda ilitengeneza ajira 146,892 ukilinganisha na mwaka 2015 ilichangia ajira 139,895.

 Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Miaka 72 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika Viwanja vya Karimjee.

Amesema sekta hiyo ina mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania kwani mwaka jana ilichangia asilimia saba ya pato la taifa huku mwaka 2015 ikichangia asilimia 6.5 ya pato hilo.

" Asilimia 75 ya watanzania wanategemea kilimo kuingiza kipato na zaidi ya asilimia 33 hawafanyi kilimo chenye tija yote imechangiwa na kutokuwa na viwanda imara," amesema.

Amebainisha kuwa Serikali inaendelea kuweka mkazo katika maendeleo ya viwanda na kwamba katika kukabiliana na changamoto zitokanazo na viwanda kuweka sera madhubuti ya kukabiliana nazo.

Amesisitiza kuwa tangu nchi ilipojiunga na UN imepata mafanikio katika nyanja mbalimbali kupitia misaada ya mashirika ya umoja na kuongeza  bado inajihusisha na usuluhishi wa migogoro pamoja na kulinda amani katika nchi zenye vita.

Kwa upande wake, Mratibu wa UN na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo Duniani (UNDP), Alvaro Rodriguez amesema bado umoja huo unakabiliana na changamoto nyingi ikiwemo ya  rasilimali hivyo umoja huo utaendelea kushirikiana na Tanzania kuhakikisha malengo iliyojiwekea yanafikiwa.


Amefafanua kuwa maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo Maendeleo ya Viwanda na Utunzaji wa Mazingira kwa Maendeleo Endelevu. 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search