Polisi wamkamata Zitto Kabwe...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na mwandishi wetu
KIONGOZI mkuu wa
chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amekamatwa na Jeshi la Polisi.
Zitto Kabwe
Amekamatwa leo majira
ya asubuhi nyumbani kwake Masaki jijini
Dar es Salaam
Afisa habari wa ACT
Wazalendo, Abdallah Khamis ameiambia Matukio360 kuwa sababu za kukamatwa kwake
ni hotuba aliyoitoa juzi katika mkuatano wake wa hadhara wa kampeni wa kumnadi
mgombea udiwani kata ya Kijichi wilayani Temeke.
“Kiongozi wetu wa ACT
Wazalendo Zitto Kabwe amekamatwa na Jeshi la Polisi muda huu(majira ya saa moja
asubuhi) akiwa nyumbani kwake na amepelekwa kituo cha Polisi Chang’ombe.
“Sababu za kukamatwa
kwake ni hotuba ya juzi(Jumapili) katika kata ya Kijichi,” amesema Khamis
Katika mkutano wa
kijichi wa kumnadi mgombea udiwani wa ACT Wazalendo, Edga Mkosamali pamoja na
mambo mengine Zitto alisema serikali inapika takwimu za ukuaji wa pato la
taifa(DGP) na si sahihi kama ambavyo taasisi za serikali zinavyotangaza.
Alisema Mkaguzi wa
Hesabu za Serikali(CAG), anapaswa kufanya ukaguzi wa mapato ya serikali kwa
Julai na Agosti mwaka huu na kuiweka
wazi kwa umma.
Zitto ambaye pia ni
mbunge wa Kigoma mjini alisema mbali na CAG kufanya ukaguzi pia Mamlaka ya
Mapato (TRA) ieleze mapato yake kwa kila idara pamoja na kuonesha marejesho na
madeni yatakayokusanywa kama mapato.
Pia alizitaka Jumuia
za Afrika Mashariki, Benki ya Maendeleo ya Afrika na Benki ya Dunia kufanya
uchunguzi maalumu wa takwimu za uchumi nchini na kwamba hatua kali zichukuliwe
dhidi ya serikali ya awamu ya tano ikigundulika kuwa takwimu juu ya ukuaji wa
pato la taifa zimepikwa.
Kampeni za uchaguzi
mdogo wa marudio wa udiwani utafanyika Novemba 26, 2017, utahusisha kata 43
nchini, Dar es salaam ikihusisha kata ya Mbweni, Kijichi na Saranga
No comments:
Post a Comment