SIDO: Wajasiliamali boresheni bidhaa ...soma habari kamili na Matukio360..#share
Na
Salha Mohamed
SHIRIKA la kuhudumia viwanda vidogo(SIDO), limewataka wajasiliamali wadogo kujiimarisha na kufunga bidhaa zao kwenye vifungashio na kuweka lebo sahihi.
SHIRIKA la kuhudumia viwanda vidogo(SIDO), limewataka wajasiliamali wadogo kujiimarisha na kufunga bidhaa zao kwenye vifungashio na kuweka lebo sahihi.
Anna Matinde kushoto akimsikiliza mmoja wa wajasiliamali
Akizungumza
na Matukio360 wakati wa kufunga maonesho ya wajasiliamali ya wakinamama jijini
Dar es Salaam, Ofisa Masoko SIDO, Antonia Masoi amesema wajasiliamali wengi
wamekuwa na changamoto ya vifungashio.
Amesema
wajasiliamali wamekuwa na bidhaa nzuri lakini kinachowakwamisha ni kutokuwa na
vifungashio vizuri na lebo sahihi.
“Bidhaa
zao ni nzuri lakini wanatakiwa kuwa wakweli kwenye lebo zao itasaidia kujenga
Tanzania ya viwanda,”amesema.
Amesema
maonesho hayo yamekuwa na watu wachache waliofika kununua na kuangalia bidhaa
kutokana na changamoto ya mvua iliyonyesha siku mbili zilizopita.
“Mvua
imewaathiri watu kuja kuona, wengine waliona uvivu kuja kutokana na mvua
kunyesha lakini hayakutangazwa tutajitahidi kutoa elimu ili washiriki zaidi
kwenye maonesho,”amesema.
Rais
wa Taasisi ya Uwezeshaji Wanawake Viccoba(Taswe), Anna Matinde amesema wajasiliamali wadogo wanapaswa kuwa karibu na
SIDO ili kukuza biashara zao.
Amesema
kupitia maonesho hayo wajasiliamali wameweza kuwasiliana na kubadilishana
mawazo katika biashara zao.
Amesema
wapo waliojitahidi kuwa wabunifu katika kutengeneza lebo pamoja na kunadi
biashara zao kupitia simu za mkononi.
“Kabla
hujaingiza bidhaa sokoni angalia lebo uliyoweka inavutia? Wengine wanaweka
majina ambayo si mazuri .
“Licha
ya kuwa na mvua lakini haikuwavunja moyo …nimefurahishwa mmejifunza na hicho
ndicho kilihowaleta si tuu kuuza bidhaa,”amesema.
Amesema
serikali iko mbioni kutenga maeneo ya usindikaji bidhaa zenye ubora
zikithibitishwa na Shirika la Viwango (TBS) na Mamlaka ya Chakula na
Dawa(TFDA).
Amesema
wajasiliamali wadogo hawataweza kuuza bidhaa zao kama hazitakuwa na TBS na TFDA
pamoja na kufungasha kwenye vifungahio visivyo na ubora.
Matinde
amesema wajasiliamali wanapaswa kuweka rekodi za mauzo na manunuzi ya kila
mwezi huku akiitaka SIDO kuandaa mafunzo ya mahesabu kwa wajasiliamali hao.
Kauli
mbiu ya maonesho hayo ni ‘Mwanamke mjasiliamali funguka shiriki Tanzania ya
viwanda' ambapo maonesho hayo yanatarajiwa kufanyika mkoani Dodoma mwakani.
No comments:
Post a Comment