Makonda amjibu waziri Lukuvi... soma habari kamili na Matukio360.. #share
Salha Mohamed
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewatoa hofu wananchi mkoani humo kuwa haitavunja nyumba ya mtu na amewataka watoa vibali, kuvitoa ndani ya mwezi mmoja tangu kupokea maombi.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
Makonda
ameyasema hayo kupitia waraka alioutoa kwa vyombo vya habari baada ya kile
kinachodaiwa kufanyika kwa uvunjaji wa nyumba za wananchi wa karne.
Ameseeza serikali inayoongozwa na Rais, Dk. John
Magufuli haivunji nyumba ya mtu bali inaendelea kurasimisha makazi kama ambavyo
ilifanya kwa
wakazi
wa Kimara kwa kuwapatia hati wananchi 6000 waliokuwa wamejenga kwenye makazi
yasiyo rasmi.
"Naomba
niseme kwenye Mkoa wa Dar es Salaam hapatakuwa na bomoa bomoa ya karne wala
nyumba ya mtu kuvunjwa, isipokuwa wananchi wanaojenga sasa ni vyema wakafuata
utaratibu kama alivyoelekeza Waziri Lukuvi, ili kuepuka kuvunjiwa nyumba ambayo
umeijenga kwa jasho jingi, na kujinyima huku ukikesha ili utimize ndoto ya kuwa
na makazi bora,"amesema.
Amesema
jitihada zinaendelea na ndivyo itakayofanyika Oktoba 27, 2017 kwa wananchi
waliojenga katika maeneo ya makongo juu.
"Naomba
kuwatoa hofu. Naomba niseme, na kama nimemuelewa vizuri alichokisema Waziri wa
Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wananchi wasiendelee
kujenga bila vibali vya ujenzi jambo ambalo linawanyima haki yao ya kukopeshwa,
kulipa kodi ya majengo, na mwishoni kuwa na miji isiyopangwa
vizuri,"amesema.
Makonda
amekiri kuwa hapo awali kulikuwa na changamoto ya upatikanaji wa vibali vya
ujenzi jambo ambalo haliwezi kuwa adhabu kwa Wananchi waliojenga miaka ya nyuma.
Amesema
"Ilifika hatua mwananchi ana Hati ya Kiwanja chake na amekamikisha michoro
kwa mujibu wa Sheria na ana fedha za kuanza Ujenzi kwa ajili ya Makazi ya
kuishi, Mwananchi huyo analazimika kufuatilia manispaa kwa zaidi ya miaka
miwili hadi mitatu bila kupata kibali cha ujenzi.
"Na
hata akipata kibali baada ya miaka mitatu na kuanza ujenzi, unakuta ndani ya
muda mfupi watakuja baadhi ya watu wa OSHA kumsimamisha kwa madai hawana
taarifa ya ujenzi jambo linalotengeneza mianya ya Rushwa,"amesema.
Amesema
mwananchi huyo akimalizana na watu wa OSHA Wanakuja baadhi ya watu wa kikosi
cha zimamoto (fire) jambo linalosababisha atafute utaratibu wa kumalizana nao,
jambo linalokera wananchi na kuwafanya wakose hamasa ya Kutafuta vibali vya
ujenzi na Hatimae kujenga kiholela.
Makonda
ameongeza kuwa kutokana na jambo hilo, baadhi ya watu wasiowaaminifu wanatumia
mwanya huo kuvamia maeneo ya watu na kujenga Kiholela na kuibua Migogoro
Mikubwa ya Ardhi.
Kutokana
na changamoto hizo, Serikali ya Mkoa imefanya kikao na wataalamu wa Ardhi
ambapo vitengo vinanavyohusika na Utoaji wa vibali vya ujenzi vinapaswa kuwa na
mfumo mmoja wa mawasiliano (one stop center) ili mwananchi atakapoomba kibali
cha ujenzi Idara zote zifikiwe kwa wakati Mmoja na kupunguza usumbufu wa
mwananchi kwenda kufuatilia vibali.
"Ili
mfumo huo uanze kufanya kazi wataalamu wangu walihitaji vitendea kazi ambavyo
nimewawezesha vifaa hivyo zikiwemo Computer 50 katika manispaa zote za Mkoa na
kuwataka kutoa vibali ndani ya mwezi Mmoja tangu kupokea maombi kutoka kwa
Mwananchi,"amesema.
No comments:
Post a Comment