'Wazazi fateni masharti ya kisukari'..soma habari kamili na Matukio360...#share
Na Abraham Ntambara
WAZAZI wenye watoto walio na maradhi ya kisukari wameshauriwa
kuhakikisha wanawahudumia kwa kuzingatia ushauri wa madaktari hususani katika
vyakula ili maisha yao yawe salama.
Msimamizi wa Mradi wa Huduma za Kisukari kwa Watoto nchini Herieh Mganga akizungumza na waandishi wa habari.
Ushauli huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Msimamizi wa
Mradi wa Huduma za Kisukari kwa Watoto
nchini Herieh Mganga wakati wa zoezi la kupima wanafunzi wa shule ya sekondari
ya wasichana Kisutu ili kubani kama wanaviashiria vya ugonjwa wa kisukari.
Zoezi hilo amablo limeratibiwa na Chama cha Wagonjwa wa
Kisukari nchini kwa Kushirikiana na Chama cha Magonjwa yasiyo ya kuambukiza,
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Tamisemi lengo ni
kufikia watoto wa kike katika maeneo mbali mbali nchini na kuwajengea ufahamu
juu ya uwepo wa uwepo wa watoto wenye ugonjwa wa kisukari.
Amesema watu wengi wamekuwa wakifariki kwa ugonjwa huo kutokana
na kukosa elimu ya jinsi ya kukabiliana nao.
“kwa hiyo hapa tupo tunapima urefu, uzito na mapigo ya moyo,
tunapima haya ili kujua kama kunaviashiria vya ugonjwa wa kisukari na magonjwa
yasiyo ya kuambukiza,” amesema.
Aidha ameeleza kuwa
tatizo hilo ni kubwa na kubainisha kuwa hadi sasa wamekwishaandikisha
vijana Zaidi ya 2488 wenye ugonjwa huo katika kilniki 34 ambazo wanazsimamia.
Mmoja wa vijana wanachama wa Chama cha Vijana wenye kisukari nchini (TBYA) Anita Bulindi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Anita Bulindi ambaye ni mmoja wa vijana ambao ni wanachama wa
Chma cha Vijana wenye Kisukari nchini (TBYA) amewataka wazazi kuamini kuwa hata
watoto wanaweza kupata maradhi hayo na kuwataka wanapokutana na hali hiyo
waione kama hali ya kawaida.
Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana Kisutu jijini Dar es Salaam, Sylvia Lymo akizungumza na waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment